Nafasi Ya Matangazo

January 28, 2025













Na Junior Mwemezi, Tume ya Madini
Leo Januari 28, 2025 Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Songwe, Chone Malembo amefunga mafunzo ya wachimbaji wadogo wa madini yaliyoanza mapema jana kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mhe. Mbarak Alhaj Batenga Wilayani Chunya mkoani Mbeya.

Akizungumza  kwenye ufungaji wa mafunzo hayo, amewataka wachimbaji hao kuzingatia Sheria na Kanuni za Madini ili uchimbaji wao uwe na manufaa huku Serikali ikipata kodi na tozo mbalimbali kupitia uimarishaji wa shughuli za uchimbaji na uchenjuaji huku wakizingatia usalama wa maisha yao na jamii inayowazunguka.

Katika hatua nyingine, Malembo amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa  na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kujipambanua katika kuwawezesha wachimbaji wadogo ili waweze kukua na kufikia viwango vya uchimbaji wa kati na mkubwa ili kufanikisha azma  ya kuongeza mchango wa Sekta ya Madini kwenye Pato la Taifa hadi kufikia asilimia 10 ifikapo mwaka 2025.

Katika hatua nyingine, Malembo amesema kuwa Serikali kupitia Tume ya Madini itaendelea kutatua changamoto za wachimbaji wadogo ikiwa ni pamoja na kuwaunganisha na Taasisi za Fedha ili kupata mikopo.
Posted by MROKI On Tuesday, January 28, 2025 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo