Nafasi Ya Matangazo

August 04, 2024

Kwenye mitandao ya kijamii inaonekana video inayosambazwa ikimwonyesha binti anayesemekana ametokea  Yombo Dovya Jiji la Dar es Salaam akidhalilishwa na kufanyiwa ukatili ambao haukubaliki kwani ni kinyume cha sheria,
maadili ya Mtanzania na Haki za Binadamu.
 
Tunapenda kutoa taarifa kuwa, Jeshi la Polisi limeshaanza kulifanyia kazi tukio hilo ovu na la kulaaniwa.
 
Aidha, Jeshi la Polisi linatoa wito kwa Wananchi wote waache kuendelea kusambaza video hiyo kwani kwa kufanya hivyo ni kosa kisheria lakini pia ni kitendo cha kuendelea kudhalilisha utu wa binadamu mwenzetu.
 
Pia tunatoa wito kwa mwenye taarifa ya kuhakikisha mkono wa sheria unawafikia kwa haraka waliofanya ukatili huu asisite kutusaidia kwa kutupa taarifa au kumpatia kiongozi yeyote yule wanayemwamini kwamba taarifa ikimfikia watu hao watapatikana haraka iwezekanavyo au toa taarifa kupitia namba hii 0699 99 88 99.
 
Imetolewa na:                                                             
David A. Misime - DCP
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Makao Makuu ya Polisi
Dodoma,Tanzania
Posted by MROKI On Sunday, August 04, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo