Nafasi Ya Matangazo

July 22, 2024

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhani akimkabidhi kadi ya Mpiga Kura, Bi. Hanifa Chija mkazi wa Mtaa wa Boma Kata ya Kimobwa, Wilayani Kasulu mkoani Kigoma baada ya kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika kituo cha Ofisi ya Mkuu wa Wilaya tarehe 21 Julai, 2024. Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura kwa mikoa ya Kigoma, Katavi na Tabora limeanza Julai 20 na litafikia ukomo Julai 26 mwaka huu.

**************
Zoezi la Uboreshaji la Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa mikoa ya Kigoma, Katavi na Tabora limeingia siku ya pili baada ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa kulizindua Julai 20,2024 katika uwanja wa Kawawa Mkoani Kigoma.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhani alipata fursa ya kukagua baadhi ya vituo vya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika Wilaya za Kasulu na Buhigwe mkoani Kigoma na kujionea hali ilivyo vituoni na mwitikio wa watu katika vituo hivyo.

Akizungumzia uboreshaji huo, Kailima  alisema hadi kufikia jana tarehe 21 Julai 2024, hapakua na changamoto yeyote iliyojitokeza katika mikoa yote ya Tabora, Kigoma na Katavi na wananchi wameendelea kujitokeza kwa wingi kujiandikisha lakini pia kuboresha taarifa zao.

Aidha, Kailima alivipongeza vyama kwa kuweka mawakala katika vituo vya uandikishaji na kuwataka mawakala hao kusaidia utambuzi kwa watu wasio raia wa Tanzania ambao watafika kwaajili ya kuandikishwa.

Kailima alitumia nafasi hiyo kuwakumbusha wananchi kuwa sasa zimesalia siku tano kati ya saba zilizopangwa kuandikisha wananchi katika mikoa hiyo ya Kigoma, Katavi na Tabora hivyo wananchi wazitumie siku zilizobaki kujitokeza na kujiandikisha.

Amesema vyama vya siasa vinawajibu wa kuwahimiza, wanachama, wafuasi wao kujitokeza kujiandikisha na kuboresha taarifa zao ili waweze kupiga kura katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhani akimkabidhi kadi ya Mpiga Kura, Frank Laswai mkazi wa Mtaa wa Murumua Kata ya Kimobwa Wilayani Kasulu mkoani Kigoma baada ya kuboresha taarifa zake katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika kituo cha Bohari ya Elimu B tarehe 21 Julai, 2024. Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura kwa mikoa ya Kigoma, Katavi na Tabora limeanza Julai 20 na litafikia ukomo Julai 26 mwaka huu.
Mwananchi akiweka saini baada ya kukamilisha ujazaji wa fomu 

Wananchi waliojitokeza kujiandikisha na wengine kuboresha taarifa zao katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura. 

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhani (kulia) akiwa katika kituo cha Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kasulu. 

Afisa mwendesha BVR, Sarah Malogo akimchukua alama za vidole Framk Laswai katika mfumo mwananchi aliyefika kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura. 

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhani (kushoto) akizungumza na baadhi ya maofisa uandikishaji katika Kituo cha Bohari ya Shule B Wilayani Kasulu. 
Baadhi ya wananchi wakiwa katika kituo cha Uboreshaji tayari kwa kuandikishwa na kuboresha taarifa zao katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura. 
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhani (kushoto) akishuhudia mwananchi akiandikshwa katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura. 
Mwananchi akiweka saini baada ya kukamilisha ujazaji wa fomu
Mwananchi akichukuliwa alama za vidole baada ya kukamilisha ujazaji wa fomu

Posted by MROKI On Monday, July 22, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo