Nafasi Ya Matangazo

December 13, 2023










Wafanyabiashara wa Soko la Bonanza-Chamwino Jijini Dodoma,wameishukuru serikali chini ya uongozi wa  *Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan* na pia Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini *Mh. Anthony Mavunde* kwa kufanikisha ujenzi wa eneo la soko la Bonanza maalum kwa ajili ya wauza mbogamboga na matunda.

Hayo yamesemwa jana wakati wa ziara ya Mbunge Anthony Mavunde kukagua ujenzi wa soko hilo na kuzungumza na wafanyabiashara wa soko la Bonanza.

Akitoa maelezo ya awali Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Soko la Bonanza *Ndg. Goha Mwagai* amesema ujenzi wa soko la mboga mboga na matunda utasaidia sana kuwafanya wafanyabiashara hao kufanya biashara katika mazingira rafiki na hivyo kutoa shukrani za pekee kwa Serikali inayoongozwa na *Mh.Dkt. Samia Suluhu Hassan* kupitia Jiji la Dodoma kwa fedha takribani *Tsh 50,000,000/*= na kwa *Mbunge Anthony Mavunde* kwa mchango mkubwa wa Nguzo za chuma zenye thamani ya *Tsh 13,300,000/=* na mabati 400 yenye thamani ya *Tsh 13,800,000/=*.

Akizungumza na wafanyabiashara hao Mbunge Mavunde amesema ni dhamira ya serikali na viongozi wote kuona wafanyabiashara hao wanafanya shughuli zao za kiuchumi katika mazingira rafiki  na hivyo watahakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati kwa manufaa ya wafanyabiashara hao.

“Ni maelekezo ya Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan kwamba wafanyabiashara lazima wapatiwe maeneo rafiki ya kufanya biashara.

Nikiwa kama Mbunge kwa kushikirikiana na Jiji la Dodoma tutahakikisha wafanyabiashara wadogo wadogo wa Dodoma wanapata maeneo rafiki na salama kwa ajili ya kufanya shughuli zao za kiuchumi

Najua hapa ujenzi haujakamilika hivyo nawaongeze matofali 1500 na saruji mifuko 100 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa kuweka sakafu ili pawe nadhifu” alisema Mavunde

Diwani wa kata ya Chamwino *Mh. Jumanne Ngede* ameahidi kusimamia mradi huo kwa karibu jwa fedha kutumika kwa malengo yaliyowekwa na si vinginevyo.
Posted by MROKI On Wednesday, December 13, 2023 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo