Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi,
utenguzi na uhamisho wa viongozi kama ifuatavyo: A: Uteuzi na Utenguzi i)Amemteua Balozi Meja Jenerali Paul Kisesa Simuli kuwa
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Uganda. ii)Amemteua Ndugu Selwa Abdalla Hamid kuwa Mkurugenzi Mtendaji
wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Ndugu Hamid anachukua nafasi ya ndugu
Athman Francis Msabila ambaye amesimamishwa kazi. Kabla ya uteuzi huu, ndugu Hamid alikuwa Meneja
Miradi, Bohari Kuu ya Dawa (MSD). iii)Amemteua Ndugu Mariam K. H. Chaurembo kuwa Mkurugenzi Mtendaji
wa Halmashauri ya Mji wa Tunduma. Ndugu Chaurembo anachukua nafasi ya Ndugu
Lena Martin Nkya ambaye uteuzi wake umetenguliwa. Kabla ya uteuzi huu, ndugu
Chaurembo alikuwa Afisa Utumishi Mkuu, Wizara ya Nishati na amewahi kuwa Mkuu
wa Wilaya ya Nanyumbu na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya
Nyang’wale. iv)Amemteua Ndugu Fabian Manoza Said kuwa Mkurugenzi Mtendaji
wa Wilaya ya Momba. Ndugu Said anachukua nafasi ya Ndugu Butamo Nuru Ndalahwa
ambaye uteuzi wake umetenguliwa. Kabla ya uteuzi huu, Ndugu Said
alikuwa Afisa Usimamizi Mkuu wa Mitihani, Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa
na amewahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu. v)Amemteua Dkt. Khamis Hassan Mwinyimvua kuwa Mwenyekiti
wa Bodi ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga, Tanzania. Dkt. Mwinyimvua ni Mhadhiri
Mwandamizi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na anachukua nafasi ya Prof. Longinus
K. Rutasitara ambaye amemaliza muda wake. B:
Uhamisho vi)Amemhamisha kituo cha kazi Dkt. Peter Maiga Nyanja,
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Muleba kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe. Ndugu Nyanja anachukua nafasi ya
Ndugu Maryam Ahmed Muhaji ambaye hivi karibuni aliteuliwa kuwa Katibu Tawala wa
Manyara. Uteuzi
na uhamisho huu unaanza tarehe 18 Desemba, 2023.
0 comments:
Post a Comment