Nafasi Ya Matangazo

December 14, 2023

 




Na John Mapepele
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki amezindua Kamati ya Kitaifa ya kuongoa shoroba za Wanyama pori katika  kongamano la kwanza  la kitaifa  la  kujadili usimamizi madhubuti wa  shoroba  hizo ili  kuleta  manufaa ya kiuchumi huku akiielekeza kamati hiyo kufanya kazi kwa kasi zaidi.


 Katika hotuba yake aliyoitoa leo Desemba 14, 2023  jijini Dar es Salaam  kwenye  kikao cha wadau zaidi ya mia mbili, Mhe. Kairuki amesisitiza kuwa katika usimamizi huo Wizara itashirikiana na wadau mbalimbali ili kufikia azma hiyo kwa kuwa jambo hilo haliwezi kutekelezwa na Wizara peke yake na amewaomba wadau wa ndani na nje ya nchi kujitokeza kushirikiana na serikali.


Amesema sambamba na zoezi hilo Serikali itaendelea kutekeleza mpango wa matumizi bora ya ardhi katika maeneo  ya shoruba  ili maeneo hayo yaweze kutumika  kikamilifu katika mawanda  mengine kama utalii wa picha hivyo kuinufaisha jamii inayozunguka maeneo hayo nan chi kwa ujumla wake.


Ameongeza kuwa kukamilika kwa matumizi bora ya ardhi pia yatasaidia  kuainisha  maeneo yatakayotumika kwa ajili ya huduma  za kijamii kama shule hospitali, kilimo na  malisho.


“Lakini kuwa na mpango wa mtumizi bora ya ardhi haitoshio tumeendelea kusisitiza  Halmashauri zetu  za wilaya na vijiji kupitia serikali za mitaa  pamoja na wenzetu kutoa elimu wa umma  ili waweze kujua  vijiji gani  vimeshaandaliwa mpango wa matumizi bora ya ardhi lakini pili kulinda yale matumizi yaliyoainishwa  ili yafuatwe” amesisitiza  Mhe. Kairuki


Amefafanua kuwa pia lengo la kikao cha Kwanza cha jukwwa la kitaifa la kuongoa  shoroba  ni kujadili suala la kuhifadhi shoroba za wanyamapori nchini ili kutekeleza Mpango wa Kuongoa na Kusimamia Shoroba 20 za Wanyamapori za Kipaumbele  nchini - 2022-2026, (Tanzania Wildlife Corridors Assessment, Prioritization and Action Plan). 


“Kikao hiki kinafanyika kwa mara ya kwanza na kimepewa jina National Corridor Forum kikilenga pamoja na mambo mengine kuwaleta pamoja wadau wa uhifadhi kutoka maeneo mbalimbali nchini ili kujadili utekelezaji wa Mpango wa Kuongoa na Kusimamia Shoroba 20 kati ya 61 za Kipaumbele  nchini (2022-2026) - (Tanzania Wildlife Corridors Assessment, Prioritization and Action Plan)” amesisitiza Mhe. kairuki


Ameyataja malengo mengine ya  kikao hicho kuwa ni pamoja na kuainisha wadau na kuweka maazimio ya nani afanye nini na wapi ili kuongoa na kuhifadhi shoroba za wanyamapori, hasa zilizo hatarini, Serikali kutoa kauli thabiti kwa wananchi kuhusu tafsiri ya maeneo ya shoroba za wanyamapori kuwa sio hifadhi na zitaendelea kuwa katika ardhi za vijiji; na kutoa kauli juu ya fursa mbalimbali zilizopo kwenye shoroba hizo, hasa utalii na biashara ya hewa ukaa ili wananchi waweze kuzitumia na kunufaika na rasilimali za wanyamapori.


Mwenyekiti wa Kamati ya kitaifa ya kuoingoa Shoroba, Linnah Kitosi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais amesisitiza kuwa jambo la kwanza kwa sasa ni kuwaelimisha wananchi waweze kuzitambua  shoroba ili wanyama waendelee kupita na wananchi waweze kufanya  shughuli zao bila kuleta  migongano  na madhara.
Posted by MROKI On Thursday, December 14, 2023 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo