Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Zanzibar (ZHC), Mwanaisha Ali Said, na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya CRDB, Stephen Adili. Kwa pamoja walisaini makubaliano ya ushirikiano kati ya Benki hiyo na Shirika la Nyumba La Zanzibar (ZHC) yenye lengo la kuwawezesha Wafanyakazi na Wafanyabiashara kuweza kununua nyumba zilizopo kwenye miradi inayosimamiwa na Shirika hilo visiwani Zanzibar, hafla hiyo ilifanyika mapema mwishoni mwa wiki. Wengine katika picha kutoka kushoto ni Kaimu Msimamizi wa Mali na Maendeleo ya Biashara wa Shirika la Nyumba la Zanzibar, na Meneja wa Biashara CRDB Kanda ya Zanzibar, Abdallar Duchi.
BENKI ya CRDB imetiliana saini na Shirika la Nyumba la Zanzibar (ZHC) ya kuwawezesha wateja wa makundi mbalimbali kumiliki Nyumba katika miradi inayosimamiwa nashirika hilo katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar.
Akizungumza mara baada ya kutiliana saini katika hafla hiyoambayo ilifanyika katika Ofisi ya Benki ya CRDB Michenzani mall, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya CRDB, Stehen Adili, alisema, makubaliano hayo yatakwenda kuwanufaisha wateja wa makundi mbalimbali kwa kupatamkopo wa thamani ya hadi shilingi Bilioni 1.
Alisema, Makundi hayo ni pamoja na wafanyakazi waMashirika au Taasisi, wanachama wa Mifuko ya Pensheni, Wajasiriamali waliojiajiri katika shughuli mbalimbali zakiuchumi, watanzania wanaoishi nje ya nchi (Diaspora) nawatanzania waishio nje ya nchi wanaomiliki hati za kusafiria zanchi nyingine.
Aidha alisema kusainiwa kwa makubaliano hayo ni muendelezo wa jitihada za benki ya CRDB katika kuwawezesha watanzania kumiliki makazi bora.
Hata hivyo, alifahamisha kuwa Benki hiyo ndio kinara wa utoajiwa mikopo ya nyumba ambapo katika mikopo yenye thaamani ya Takribani Bilioni 593.76 iliyotolewa na taasisi za fedha ambapo benki ya CRDB imetoa takribani bilioni 197.70 sawa naasilimia 33.3.
Hivyo, alisisitiza kuwa Benki itaendelea kushirikiana na ZHC kwa kufanya nao kazi pia alilipongeza shirika hilo kwa kazinzuri wanayoifanya katika kuboresha hali ya makazi visiwani Zanzibar, pia aliipongeza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katikautekelezaji na ufanikishaji wa miradi hiyo ya uongozi waawamu ya nane ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa barazala Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi katika kukuza hali yamakazi ya wananchi wa Zanzibar.
‘Benki nasi tunaungana nae katika jhitihada hizi kwa kuhakikisha kuwa tunawawezesha wananchi wa Zanzibar naduniani kote kuweza kumiliki makazi bora kwa gharama nafuu’ alisema.
Nae, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Zanzibar (ZHS), Mwanaisha Ali Said, alisema, makubaliano hayoyatawawezesha kukamilisha vyema nyumba hizo sambamba nakuipongeza benki ya CRDB kwa kuendeleza umoja huo.
Aidha alisema fursa hiyo itawaengezea kufanya kazi katika miradi mipya inayotarajiwa kufanyika kupitia njia ya malipo yataslimu, kulipa kwa awamu na njia ya mkopo ambapo alisemanjia ya mkopo ilikuwa bado haijafanya vizuri, hivyo kwa kufikiwa kwa makubaliano hayo shirika la nyumba litawasaidia kupata wateja katika njia ya tatu yaani kwa wateja kupata mikopo.
Hivyo, alisema makubaliano hayo yatagusa miradi yote inayotarajiwa kujengwa baada ya Mombasa na wanampango kujenga maeneo ya Nyamanzi na kuwataka wananchi kupeleka maombi yao kwa kutumia nyumba za Mfikiwa Pemba sambamba na kuahidi kuwa shirika linaendelea kutatua changamoto mbalimbali kwa ajili ya makazi ya nyumba iliyokuwa bora zaidi.
Mapema, Meneja wa Benki ya CRDB kanda ya ZanzibartAbdalla Duchi, alisema Benki yao itaendelea kufanya kazi naserikali pamoja na taasisi mbalimbali ili kuona wananchi wanapata huduma za kimaendeleo kupitia benki hiyo.
Benki ya
0 comments:
Post a Comment