Watu 47 wameripotiwa
kupoteza maisha na wengine 85 kujeruhiwa katika Vijiji vya Katesh na Gendabi
wilayani Hanang mkoani Manyara baada ya
Mafuriko kuyakumba maeneo hayo usiku wa mkuamkia Disemba 3,2023.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga watu zaidi wanahofiwa kufukiwa na matope baada nyumba na makazi yao kusombwa na mafuriko na maporomoko ya udongo kutoka Mlima Hanang’.
Eneo kubwa lililoathiriwa na mafuriko hayo ni kata ya Gendabi na Katesh ambapo ndipo makao makuu ya Wilaya ya Hanang’.
Nyumba za watu zimezingirwa na mafuriko na miti iliyosombwa na mafuriko kutoka sehemu ya Mlima Hanang yamesababisha barabara ya Katesh kwenda Singida kushindwa kupitika kwa muda.
Wakazi wa Hanang’
wamesema hawajawahi kushuhudia hali kama hiyo na kwamba kwao hilo ni janga
kubwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kufuatia tukio hilo na kuzitaka mamlaka zote zihamishie nguvu wilayani Hanang kutoa msaada
0 comments:
Post a Comment