Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa
viongozi na kuvunja bodi kama ifuatavyo:
1.
Amemteua Balozi James Gilawa Bwana kuwa Balozi wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Afrika kusini. Balozi Bwana anachukua
nafasi ya Balozi Meja Jenerali Gaudence Salim Milanzi ambaye amestaafu.
2.
Amemteua Balozi Said Hussein Massoro kuwa Balozi wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Kuwait.
Balozi
Massoro anachukua nafasi ya Balozi Said Shaib Mussa ambaye aliteuliwa kuwa
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
3.
Amemteua Bw. Kaimu Abdi Mkeyenge kuwa Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC). Kabla ya uteuzi huu Bw. Mkeyenge
alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC).
Bw.
Mkeyenge anachukua nafasi ya Dkt. Elirehema Doriye ambaye atapangiwa kazi
nyingine.
Uteuzi
huu unaanza mara moja.
4.
Amevunja Bodi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA) kuanzia tarehe 07 Novemba, 2023.
0 comments:
Post a Comment