November 29, 2023

DODOMA KINARA MBIO ZA MWENGE 2023








Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amebainisha kupanda chati kutoka nafasi ya 22 kati ya 31 kwa mwaka 2022 na kushika nafasi ya 1 kati ya mikoa 31 kwa 2023 katika Ukaguzi wa miradi, uzinduzi wa Miradi na Shamrashamra za namna viongozi walivyoshiriki katika kukimbiza Mwenge wa Uhuru Mkoani Dodoma.

Senyamule amebainisha hayo katika Kikao kazi kilichofanyika leo Novemba 29/2023 katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jengo la Mkapa kilichowajumuisha Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri na Wataalam mbalimbali wa  Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Kikao hicho kimefanyika huku kikiwa na ajenda mbalimbali ikiwemo maandalizi ya msimu wa kilimo, tathmini ya upandaji Miti na tathmini ya Mwenge wa Uhuru ikijumuisha utolewaji wa matokeo ya Mwenge wa Uhuru uliokimbizwa Mkoani humo mnamo mwezi Septemba mwaka huu.

"Tumetumia siku ya leo kufanya tathmini Kama ambavyo huwa tunafanya Miaka yote ya kuona namna ambavyo tumetekeleza ubora wa Miradi na vigezo vingine vilivyowekwa katika shughuli za Mwenge wa Uhuru.

"Tunamshukuru Mungu   Halmashauri 5 za Dodoma Jiji,Kondoa DC na TC, Mpwapwa na Kongwa zimeingia katika 10 bora ya Taifa, Mwaka Jana 2022 Mkoa ulishika nafasi ya 22 hatukupendezwa na matokeo hayo Kama Makao makuu ya Nchi, tulipeana Shime ya kuifaharisha Dodoma na tukaungana kupambania Mkoa na tunamshukuru Mungu kwa mara ya kwanza tumeshika nafasi ya Kwanza Kitaifa tumeifahalisha Dodoma na Makao makuu ya Nchi", amebainisha Senyamule.

Katika kuelekea msimu wa kilimo Afisa kilimo wa Mkoa wa Dodoma Bw. Abraham amesema Wapo tayari kwa uzinduzi wa msimu wa kilimo unaotarajiwa kuzinduliwa Novemba 29 mwaka huu Katika kata ya mazae Wilayani Mpwapwa.

Aidha ametaja jitihada zinazofanywa na Mkoa katika kuhakikisha wananchi na wakulima wa Mkoa huo wanapata mazao bora, ikiwa ni pamoja na kupima Afya za udongo, kuhakikisha upatikanaji wa mbegu bora na za kisasa pamoja na kuwahamasisha wakulima kutumia mbolea na kuachana na dhana za kuwa mbolea za kisasa zinaathiri udongo na rutuba ya mazao.

No comments:

Post a Comment