November 28, 2023

WALIOFARIKI KUONDOLEWA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA

Mkurugenzi wa Habari na Elimu ya Mpiga Kura kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bi. Giveness Aswile akijadili jambo na Lazarus  Madembwe Mkuu wa TEHAMA Tume ya Taifa ya Uchaguzi  wakati akikagua vifaa katika zoezi la uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura kwenye kituo cha Masempele kata ya Ng'ambo mkoani Tabora leo Novemba 28,2023.

Mkurugenzi wa Habari na Elimu ya Mpiga Kura kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bi. Giveness Aswile akisalimiana na Mkurugenzi wa Daftari na Tehama Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Geofrey Mpangala mara baada ya kuwasili katika kituo cha Masempele alipokagua uboreshaji wa Daftari la wapiga kura kata ya Ng'ambo mkoani Tabora.

Mkurugenzi wa Habari na Elimu ya Mpiga Kura kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bi. Giveness Aswile akipata maelezo kutoka kwa Mohammed Chilongani  BVR Kit Operator katika kituo cha  shule ya sekondari ya Kaze wakati alipotembelea vituo vya uboreshaji wa Daftari la wapiga kura kata ya Ng'ambo mkoani Tabora.

**************

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeeleza kuwa inatarajia kuondoa taarifa za watu waliofariki katika uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Habari na Elimu ya Mpiga Kura kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bi. Giveness Aswile, wakati akizungumzia juu ya zoezi la Uboreshaji wa Majaribio wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura mara baada ya kutembelea katika vituo mbalimbali vilivyopo kata ya Ng'ambo Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, Mkoani humo.

Aswile ameeleza kuwa kuna vituo baadhi walivyopita na kukuta Mwandishi msaidizi katika eneo hilo ameorodhesha majina ya watu ambao wamepoteza maisha, na majina yao akiwa ameyapata kutoka kwa mwenyekiti wa Serikali za mitaa jambo ambalo ni zuri lakini hakuna namba zao za kadi ya mpiga kura za marehemu.

Ameeleza kuwa jambo hilo la kuwaondoa watu waliofariki katika daftari la kudumu la wapiga kura ni jambo ambalo wanapaswa kuliangalia namna gani watafanya ili kuboresha kwa kuwatumia Wenyeviti wa mitaa kuliko kusubiria mpiga kura aje kutoa taarifa za mtu aliyefariki.

"Katika baadhi ya tamaduni zetu kuzungumzia habari za watu waliofariki ni ngumu ni kama kuwakumbushabo yaliyopita na hivyo kuifanya njia hiyo kuwa ngumu kupata taarifa za waliofariki". Amesema Aswile

Kwa upande mwingine Aswile ameeleza kuwa kuna baadhi ya changamoto walizozipata katika zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, ambapo kuna baadhi ya watu wanaoboreshwa kwenye fomu 5 (a) wengi wao ni waliohamia na waliopoteza kadi kwa sababu waliohamia wanakuja na kadi na aliyepoteza kadi hawana hata namba wala hawakumbuki jina au anakumbuka jina la mwisho pekee.

"Sisi baadhi ya watanzania  tuna utamaduni ambao utafiti unapaswa ufanyike inakuwaje mtu hakumbuki jina lake alilojiandikishia na kituo alichojiandikisha inawezekana kweli ukasahau jina lako".

Amesema kuwa kuna watu ambao wanatafutwa kwenye mfumo ili waweze kuboresha kupitia fomu 5A bahati mbaya wengine hawakumbuki jina walilojiandikisha awali hivyo mashine kutumia muda mwingi kutafuta .

"Changamoto hii haitatuliwi na vifaa Tume itakaa kuona namna ya kuwezesha kumpata mtu aliyeko kwenye mfumo kwa urahisi kuhakikisha tunaenda vizuri katika zoezi kubwa linalokuja la uchaguzi" amesema Aswile

No comments:

Post a Comment