MBUNGE wa Jimbo la Chalinze, Mkoani Pwani, Ridhiwan Kikwete leo ametembelea na kuona maendeleo ya Ujenzi wa Mradi wa Bwawa Kubwa la Maji litakalogharimu Shilingi Milioni 900 huko Mjembe, Kwamduma.
Bwawa hilo kubwa linajengwa na Wakala wa Maji Vijijini-RUWASA.
Pindi litakapokamilika litapeleka maji katika Vitongojj vyote vya kijiji cha Kwamduma.
Aidha Mbunge huyo ameongea na wananchi na kuwaasa kujikinga na kupambana na ugonjwa wa UVIKO 19 na kujitokeza kwa wingi kwenda kuchanja.








0 comments:
Post a Comment