August 04, 2021

MBUNGE WA CHALINZE AKAGUA UJENZI WA BWAWA LA MAJI KWA MJEMBE


MBUNGE wa Jimbo la Chalinze, Mkoani Pwani, Ridhiwan Kikwete leo ametembelea na kuona maendeleo ya Ujenzi wa Mradi wa Bwawa Kubwa la Maji litakalogharimu Shilingi Milioni 900 huko Mjembe, Kwamduma.

Bwawa hilo kubwa  linajengwa na Wakala wa Maji Vijijini-RUWASA.

Pindi litakapokamilika litapeleka maji katika Vitongojj vyote vya kijiji cha Kwamduma. 

Aidha Mbunge huyo ameongea na wananchi na  kuwaasa kujikinga na  kupambana na ugonjwa wa  UVIKO 19 na kujitokeza kwa wingi kwenda kuchanja.



No comments:

Post a Comment