MTUMISHI wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo,Modest Mfutakamba Mfilinge (pichani) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Desemba 24,
2016 jijini Dar es Salaam.
Kufuatia msiba huo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Nape Nnauye amemtumia salamu za rambirambi, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Elisante Ole Gabriel pamoja na familia ya Mfilinge kufuatia kifo hicho.
Waziri pamoja na
watendaji wa Wizara wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha mwanahabari
huyo kwani ni pigo katika tasnia ya habari nchini.
Waziri Nape amepokea kwa
masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha mwanahabari huyo na ameeleza kuwa, kifo
chake ni pigo katika tasnia ya habari hususani katika picha kwasababu Marehemu
wakati wa uhai wake ametoa mchango mkubwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari
ikiwemo magazeti ya Majira, Business Times, The Guardian, Nipashe na Mwananchi
na The Citizen.
Mungu azilaze roho za Marehemu mahali
pema peponi. Amina.
No comments:
Post a Comment