Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ametuma salamu za rambirambi kwa familia,
ndugu, jamaa wapiga picha pamoja na Wanahabari wote nchini kufuatia kifo cha mwanahabari
na mpiga picha Mpoki Bukuku kilichotokea leo katika Taasisi ya Mifupa (MOI)
Mhe. Nape Nnauye pamoja na
watendaji wa Wizara wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha mwanahabari
huyo kwani ni pigo katika tasnia ya habari nchini.
“Nimepokea
kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha mwanahabari Mpoki Bukuku. Kifo chake
ni pigo katika tasnia ya habari hususani katika picha , nimehuzunishwa sana kwa
sababu Marehemu wakati wa uhai wake ametoa mchango mkubwa kwenye vyombo
mbalimbali vya habari ikiwemo magazeti ya Majira, Business Times , The Guardian , Nipashe
na Mwananchi na The Citizen.”
Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi. Amina.
No comments:
Post a Comment