December 06, 2016

SAIDA KAROLI ALIVYOPAGAWISHA TAMASHA LA CHAKALE DHAHABU JIJINI DAR ES SALAAM

Msanii wa Muziki wa Asili Saida Karoli mwishoni mwa wiki alitia fora kwa kutoa burudani kali na ya aina yake wakati akiongoza safu ya burudani za asili katika Tamasha kubwa la 'CHAKALE DHAHABU lililofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 

Tamasha la CHAKALE DHAHABU liliandaliwa na kampuni ya Seree limefanyika kwa mara ya kwanza nchini na kuwakutanisha machief wa makabila mbalimbali nchini pamoja na waliohudhuria kula vyakula vya asili.
 Mmoja wa wasanii wa Saida Karoli akionesha mbwembwe zake.
 Kundi la vijana wa Kimaasai wakitoa burudani
 Mmoja ya kundi la utamaduni likisubiri kutumbuiza katika tamasha hilo.
Ester Baruti nae alikuwepo katika tamasha hilo. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.

  Picha zilipigwa katika makazi ya Machifu
 Hili pozi la hawa jamaa nalo kama burudani flani hivi
MC wa tamasha hilo alikuwa Antonio Nugaz 'Rafiki Mtembezi' 
 Baadhi ya waalikwa wakiwa na Mwandaaji wa tamasha hilo Sabina Kaphipa (katikati).
Chifu  Charles Kaphipa   wa Bukumbi Mwanza akizungumza wakati wa tamasha la utamaduli la Chakale Dhahabu lililofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam ambapo alieleza kuwa mmomonyoko wa maadili katika jamii na kusahau mila na desturi ndio chanzo cha kutokea matukio ya kikatili nchini. Kushoto ni Chifu Deus Masanja wa jamii ya Sizakiushahi Wilaya ya Bunda na kulia ni Chifu Charles Itale wa Jamii ya Bujashi Wilayani Magu.
Chifu  Charles Kaphipa   wa Bukumbi Mwanza akizungumza wakati wa tamasha la utamaduli la Chakale Dhahabu lililofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam ambapo alieleza kuwa mmomonyoko wa maadili katika jamii na kusahau mila na desturi ndio chanzo cha kutokea matukio ya kikatili nchini. Kushoto ni Chifu Deus Masanja wa jamii ya Sizakiushahi Wilaya ya Bunda. 
 Baadhi ya watu waliohudhuria tamasha hilo
  Burudani ya kutoka ngoma ya Wakwerwe mkoani Pwani nayo ilikonga nyoyo za watu.
 Kikosi kazi cha Saida Karoli kikishambulia jukwaa
 Saida Karoli akifanya yake
 Mwandaaji wa tamasha hilo, Sabina Kaphipa alishindwa jizuia na kuingia uwanjani
Burudani iliendelea
 Huyu nae alitoa vioja vya mwaka
 Sabina akizungumza na Machief wa jamii za Kimaasai
Picha mbalimbali za pamoja zilipigwa

No comments:

Post a Comment