Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya
Mapato Tanzania ( TRA), Alphayo Kidata akikata utepe kama ishara rasmi ya
uzinduzi wa ofisi mpya ya TRA iliyoko Kimara Mwisho leo Oktoba 26, 2016,
Kushoto kwake ni Kamishna wa Kodi za Ndani TRA, Elijah Mwandumbya pamoja na
Wakurugenzi wengine wa TRA wakishuhudia tukio hilo
Meneja wa TRA Kinondoni, Wallace Mnkande (anayeongea kwa vitendo) akitoa maelezo ya kituo hicho kipya
kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata
(aliyeketi) wakati wa uzinduzi wa ofisi hiyo. Wengine kutoka kulia ni Kamishna
wa Kodi za Ndani TRA, Elijah Mwandumbya, Naibu Kamishna wa Kodi za Ndani,
Abdul Zuberi, Meneja wa Majengo Gerald Mwikuka, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Gerald Mwanilwa na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi,
Richard Kayombo.
Kamishna wa Kodi za Ndani TRA, Elijah
Mwandumbya akimweleza jambo Kamishna Mkuu wa TRA, Alphayo Kidata
alipotembelea ofisi mpya za TRA Kimara Mwisho kwa ajili ya uzinduzi rasmi wa
ofisi hiyo.
Meneja wa TRA Kinondoni,
Wallace Mnkande akimwonesha jambo Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA), Alphayo Kidata (kushoto kwake) alipotembelea ofisi ya TRA Kimara
Mwisho wakati wa uzinduzi huo uliofanyika tarehe 26 Oktoba 2016
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya
Mapato Tanzania ( TRA), Alphayo Kidata akisalimiana na baadhi ya walipakodi
waliofika katika ofisi mpya ya TRA iliyoko eneo la Kimara Mwisho ili kuhakiki
Namba zao za Utambulisho wa Mlipakodi –TIN wakati wa uzinduzi wa ofisi hiyo.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya
Mapato Tanzania ( TRA) , Alphayo Kidata akiongea na baadhi ya
walipakodi waliofika katika ofisi mpya ya TRA-Kimara Mwisho ili kuhakiki Namba
zao za Utambulisho wa Mlipakodi –TIN wakati wa uzinduzi wa ofisi hiyo.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya
Mapato Tanzania ( TRA), Alphayo Kidata – (Mwenye suti ya bluu
katikati) pamoja na Kamishna wa Kodi za Ndani TRA , Elijah Mwandumbya
(Kushoto kwake) wakiwa katika picha ya pamoja na walipakodi waliofika katika
Ofisi Mpya ya TRA Kimara ili kuhakiki Namba zao za Utambulisho wa Mlipakodi
–TIN. Ofisi hiyo imezinduliwa leo tarehe 26 Oktoba 2016 na Kamishna Mkuu wa TRA
ili kuwafikia wananchi kwa karibu zaidi na kuboresha huduma mbalimbali za Kodi.
*******************
KATIKA jitihada za kuboresha
huduma kwa walipakodi na kuzifikisha huduma hizo kwa karibu
zaidi Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ( TRA),
Alphayo Kidata amezindua ofisi mpya ya TRA katika eneo la Kimara
Mwisho jijini Dar es Salaam leo.
Ofisi hiyo itatoa huduma zote za
kikodi ikiwemo usajili na uhakiki wa Namba za Utambulisho wa
Mlipakodi –TIN, Usajili wa Kodi ya Ongezeko la Thamani-VAT, Malipo ya Kodi za
Magari, Kodi zote za Mapato zikiwemo Kodi za Makampuni, Watu Binafsi,
Wafanyakazi (PAYE), Kuendeleza Ufundi Stadi - SDL, VAT, Ushuru wa Stampu na
huduma nyingine za kikodi.
Akizungumza na walipakodi
waliofika katika ofisi hiyo kupata huduma wakati wa uzinduzi, Bw. Kidata
aliwashukuru kwa mwitikio wao katika zoezi la uhakiki wa taarifa za TIN ambao
utaisaidia Mamlaka kupata idadi sahihi ya walipakodi ili kuondoa walipakodi
hewa ikiwa ni pamoja na kuboresha huduma za ulipaji kodi.
“Zoezi hili litaongeza ufanisi
katika suala zima la usimamizi na ukusanyaji kodi kwa kiwango cha juu” Alisema Kidata
Kamishna Mkuu wa TRA aliwataka
walipakodi hao wanaoishi maeneo ya karibu na ofisi hiyo mpya ya TRA iliyopo
Kimara Mwisho kuendelea kujitokeza kwa wingi ili kupata huduma mbalimbali za
kikodi ikiwemo uhakiki wa taarifa zao TIN kabla ya tarehe ya mwisho wa zoezi
hilo kwa Mkoa wa Dar es Salaam ambayo ni tarehe 30 Novemba 2016.
Aidha Kamishna wa Kodi za
Ndani TRA, Elijah Mwandumbya alisema TRA imejipanga kuhakikisha inaendelea
kuboresha huduma zake na kuwafikia walipakodi kwa ukaribu zaidi ili kuondoa
usumbufu na kuokoa muda wa upatikanaji wa huduma hizo.
“TRA kwa kuhakikisha
walipakodi wanapata huduma iliyo bora imeanzisha vituo vingi vya kodi katika
jiji la Dar es Salaam na nchi nzima ili walipakodi wapate huduma
stahiki na ya haki na kuiwezesha Serikali kupata mapato yake kwa mendeleo ya
Taifa letu” Alisema, Mwandubya.
0 comments:
Post a Comment