KUFUATIA kitendo cha askari namba F. 3016 SGT Talib Hamad Kassim ambaye tayari
amefukuzwa kazi na Jeshi la Polisi kwa kitendo chake cha kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa raia wa kigeni mjini
Zanzibar, Jeshi la Polisi nchini linalaani vikali tabia hiyo na kwamba ni tabia
ya askari binafsi na siyo maadili ya askari wa Jeshi la Polisi.
Msemaji wa Jeshi la Polisi,Kamishna Msaidizi wa
Polisi, Advera Bulimba, Kutokana na kitendo hicho, tayari Jeshi la Polisi limemfukuza
kazi askari huyo na atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria. Aidha,
Jeshi la Polisi litaendelea kuchukua hatua kali dhidi ya askari wake yeyote
atakayekiuka maadili yake ya kazi.
Jeshi la Polisi nchini halitamuonea muhali askari
yeyote atakayekwenda kinyume na maadili ya kazi na kutenda vitendo binafsi
vinavyo lifedhehesha au kulitia dosari Jeshi la Polisi.
No comments:
Post a Comment