Meneja Masoko
wa Tbl Group ,George Kavishe (kulia) na Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Konyagi
Tanzania (TDL) Devis Deogratius (kushoto) wakiteta jambo wakati walipokuwa
wakiwaonyesha waandishi wa habari( hawapo pichani) moja ya
zawadi ya magari wakati wa kutambulisha wa zawadi za kampeni
iliyoendeshwa kwa wasamabazaji wake ya NUNUA,UZA,SHINDA NA KONYAGI
iliyodumu kwa muda wa wiki 12 iliyoanza Julai mpaka Septemba 2016 hafla hiyo
ilifanyika leo kwenye ofisi za Konyagi Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
Moja ya zawadi
ya magari ya Kampeni ya Nunua Uza ,Shinda na Konyagi kwa wasambazaji wake nchini
yaliyotambulishwa kwa waandishi wa habari kwenye ofisi za Tanzania
Distilleries Limited(TDL) leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Meneja
Mkuu wa Kampuni ya Konyagi Tanzania (TDL) Devis Deogratius (kushoto) akiongea
na waandishi wahabari wakati wa kutambulisha zawadi za kampeni
iliyoendeshwa kwa wasamabazaji wake ya NUNUA,UZA,SHINDA NA KONYAGI
iliyodumu kwa muda wa wiki 12 iliyoanza Julai mpaka Septemba 2016.Katikati ni
Kaimu meneja wa huduma za masoko wa Konyagi, George Kavishe. hafla hiyo
ilifanyika leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Meneja wa
huduma za masoko wa Konyagi George Kavishe (kulia) akiongea na waandishi
wahabari wakati wa kutambulisha zawadi za kampeni iliyoendeshwa kwa
wasamabazaji wake ya NUNUA,UZA,SHINDA NA KONYAGI iliyodumu kwa muda wa
wiki 12 iliyoanza Julai mpaka Septemba 2016 hafla hiyo ilifanyika leo kwenye
ofisi za Konyagi Chang’ombe jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Kaimu Meneja Mkuu
wa Kampuni ya Konyagi Tanzania (TDL) Devis Deogratius
Meneja Masoko
wa TBL Group, George Kavishe akijaribu kuendesha moja zawadi ya gari wakati wa
kutambulisha kwa waandishi wahabari (hawapo pichani) zawadi za kampeni
iliyoendeshwa kwa wasamabazaji wake ya NUNUA,UZA,SHINDA NA KONYAGI
iliyodumu kwa muda wa wiki 12 iliyoanza Julai na inakaribia kuika mwisho, hafla
hiyo ilifanyika leo kwenye ofisi za Konyagi Chang’ombe jijini Dar es Salaam. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
KAMPUNI ya Tanzania Distilleriers Limited (TDL) inayotengeneza na kusambaza kinywaji maarufu cha Konyagi na jamii zake, leo imezitambulisha zawadi za kampeni iliyoendeshwa kwa wasambazaji wake kwa kampeni iliyojulikana kama NUNUA, UZA, SHINDA NA KONYAGI iliyodumu kwa muda wa wiki 12. Toka Mwanzo wa Julai mpaka Mwisho wa mwezi Septemba 2016.
Akizungumza
katika hafla hiyo iliyofanyika katika Ofisi za Konyagi Changombe - Dar es
salaam, Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni ya TDL, Bwana Devis Deogatius
“Tunazitambulisha zawadi hizi kwa ili watu waamini kwamba tulichohaidi tumetekeleza,
tunafahari kubwa kwa jinsi kampeni hii ilivyoongeza chachu ya manunuzi na
wasambazaji wetu walifanya kazi nzuri .
Tutakabidhi
magari haya katika hafla mbili, droo ya kwanza itafanyika Mbeya siku ya Ijumaa
tarehe 07 Oktoba katika ukumbi wa Mbeya City Pub na itahusisha wasambazaji wa
mikoa ya Kusini na Nyanda za juu Kusini.
Droo ya
pili itafanyika Mjini Moshi tarehe 13 Oktoba katika ukumbi wa Kili Home na
itahusisha wasambazaji wa Kanda ya Kaskazini na Kanda ya Magharibi mikoa ya
Kanda ya Ziwa.
Dhumuni kuu la
kampuni yetu ya TDL kuendesha kampeni hii ni kwanza kabisa kuwainua wasambazaji
wa bidhaa zetu kwa kuwapa nafasi ya kushinda vitendea kazi.
Tuliwapa
malengo na waliofikia wataingizwa kwenye droo ili kujishindia magari
mapya mawili ya usambazaji (Eicher 3 Tonne Truck zenye thamani ya zaidi ya
milioni 110). Tunaamini kwa magari haya wasambazaji wetu wataweza kurahisishwa
utendaji wao ndani ya maeneo yao ya mauzo”
Pia, kupitia
shindano hili tutaweza kuchangia maendeleo ya kichumi nchini pamoja na jamii
kwa ujumla. Aliendelea kusema.
Naye Kaimu
Meneja wa huduma za Masoko wa Konyagi Bwana George Kavishe “ ni faraja yetu
kubwa tukiona huduma za bidhaa zetu zikiboreshwa kila mara na kuwafanya
wasambazaji wetu wawe na motisha ya kuendelea kufanya kazi na sisi
tunawashukuru sana kwa wale waliofanikisha programu hii. Maandalizi yote ya
droo kwenye mikoa ya Mbeya na Kiimanjaro yamekamilia na tupo imara.
No comments:
Post a Comment