Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mama Samia Suluhu Hassan
akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la 30 la Taasisi ya Taifa ya
Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR), lililoanza leo Oktoba 4 na
kilelele chake kukoma Oktoba 6,2016 katika Ukumbi wa Mikutano wa
Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
***********
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amelalani vikali
mauaji ya watafiti WAWILI wa kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Selian cha Arusha na
dereva MMOJA waliokuwa kazi katika kijiji cha Mvumi Makulu wilayani Chamwino
mkoani Dodoma.
Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo leo 4-Oct-2016 wakati akifungua kongamano ya 30 la Kimataifa la
Wanasayansi lililoandaliwa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya
Binadamu (NIMR) katika ukumbi wa
Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Makamu wa
Rais amesema kuwa tukio hilo ni baya na amewahakikishia watafiti wanaoshiriki
kongamano hilo kuwa serikali itachukua hatua stahiki kwa watu waliofanya kitendo hicho cha kinyama ili
kukomesha tabia hiyo.
“Haiwezekani
hata kidogo watu kufanya mauaji hayo ya kikatili na waachwe bila kuchukuliwa hatua
kali za kisheria alisisitiza Makamu wa Rais”
Akizungumzia
masuala ya utafiti, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema serikali inatambua
kazi nzuri inayofanywa na watafiti hao hivyo serikali itaendelea kutoa mchango
wake wa hali na mali ili kuhakikisha watafiti hao wanafanya kazi zao kwa ufanisi
unaotakiwa.
Makamu wa
Rais pia amewahimiza wafadhili waendelee kusaidia watafiti hasa wanaofanya tafiti
za afya nchini kwa sababu tafiti hizo zitasaidia kwa kiasi kikubwa namna ya kukabiliana
na magonjwa mbalimbali.
Amesema kuwa
watafiti wanamchango mkubwa katika kuleta maendeleo kupitia matokeo ya tafiti
zao nchini hivyo jitihada hizo ni muhimu zikaimarishwa ipasavyo.
Kongamano hilo la 30 la Kimataifa la
Wanasayansi lililoandaliwa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya
Binadamu -NIMR- linajumuisha watafiti
mbalimbali kutoka Ulaya,Afrika na Amerika.
Katika
kongamano hilo, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu
Hassan ameshiriki katika zoezi utoaji wa tuzo kwa wanasayansi waliofanya tafiti
mbalimbali za afya nchini.
Baadhi
ya Washiriki kutoka sehemu mbalimbali ndani nje ya nchi wakisikiliza
hotuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mama Samia
Suluhu Hassan wakati wa ufunguzi wa Kongamano la 30 la Taasisi ya Taifa
ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR), lililoanza leo Oktoba 4 na
kilelele chake kukoma Oktoba 6,2016 katika Ukumbi wa Mikutano wa
Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi
Mkuu,Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Dkt Mwele
Malecela akizungumza mapema leo,alipokuwa akimkaribisha Makamu wa Rais
Mama Samia Suluhu Hassan,wakati wa ufunguzi wa Kongamano la 30
lililoanza leo Oktoba 4 na kilelele chake kukoma Oktoba 6,2016 katika
Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es
Salaam.Katika kongamano hilo kauli mbiu yake ni “Uwekezaji katika tafiti
zenye ubunifu ili kufikia malengo endelevu ya dunia.”. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Dkt Mwele alieleza pia Mada zitakazojadiliwa ndani ya kongamano hilo
kuwa zitajikita zaid kwenye maeneo kama vile 1. Mkakati wa kuboresha
afya ya uzazi, ya mama, watoto wachanga na vijana. 2. Magonjwa sugu
yasiyoambukiza na changamoto zake,3. Kuendeleza mafanikio yaliyopatikana
katika mapambano dhidi ya UKIMWI, kifua kikuu na malaria,4. Usalama wa
Maji, Usafi wa mazingira na usafi binafsi,5. Mkakati wa afya moja katika
kudhibiti magonjwa ya milipuko,pamoja na 6. Magonjwa ya kitropiki
yasiyopewa kipaumbele.
Baadhi ya Washiriki wa kongamano hilo kutoka sehemu mbali mbali ndani na nje ya chi wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo,ambapo mada zaidi ya 200 zitawasilishwa na kujadiliwa kwa siku tatu.
Baadhi ya Washiriki wa kongamano hilo kutoka sehemu mbali mbali ndani na nje ya chi wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo,ambapo mada zaidi ya 200 zitawasilishwa na kujadiliwa kwa siku tatu
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mama Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Naibu Waziri wa Afya,Dkt.Hamis Kigwangala,alipokuwa akiwasili katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam leo,kwa ajili ya uzinduzi wa Kongamano la 30 la Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR),pichani kushoto ni Mkurugenzi Mkuu,Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Dkt Mwele Malecela Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mama Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu,Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Dkt Mwele Malecela,alipokuwa akiwasili katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam leo kufungua Kongamano la 30 la Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR),pichani kati ni Naibu Waziri wa Afya,Dkt.Hamis Kigwangala.
Baadhi ya Washiriki wa kongamano hilo kutoka sehemu mbali mbali ndani na nje ya chi wakiimba wimbo wa Taifa kabla ufunguzi wa Kongamano hilo,lililoanza leo jijini Dar.

BOFYA HAPA KUSOMA HOTUBA YA MAKAMU WA RAIS KUHUSU KONGOMANO HILO BOFYA HAPA
KUSOMA HOTUBA YA MKURUGENZI MKUU WA NIMR DKT MWELE MALECELE BOFYA HAPA
KUSOMA HOTUBA YA MKURUGENZI MKUU WA NIMR DKT MWELE MALECELE BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment