Moja kati ya
wajasiriamali watakaokuwepo katika maonyesho ya wajasiriamali ya Airtel
FURSA, Bi Theresia Maliatabu akiandaa bidhaa zake za picha za Sanaa
nyumbani kwake mbagala rangi tatu. Theresia
ni moja kati ya wafanyafanya biashara waliowezeshwa na mradi wa kuinua
vijana wa Airtel FURSA
****************
Mkuu wa wilaya ya kinondoni Mh. Ally Hapi anatarajiwa kufungua maonyesho ya wajasiliamali mbalimbali wanaodhaminiwa na Mpango wa Airtel FURSA yatakayofanyika
ijumaa hii katika viwanja vya ofisi za Airtel makao makuu Morocco jijini Dar es Salaam kuanzia saa nne asubuhi hadi jioni.
Airtel kupitia mpango wake wa
Airtel FURSA tunakuwezesha, umeandaa mpango utakaowawezesha
wajasiriamali hao ambao awali waliowazezwa kupitia mpango wake wa
Airtel FURSA ili waweze kuonyesha biashara zao kwa lengo la kuwawezesha
wafanyabiashara kutangaza na kupata masoko ya biashara
zao ili kukuza biashara na mitaji yao.
Akiongea
juu ya maonyesho hayo, Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando
alisema “ tumeonelea ni vyema kujipanga katika kuendeleza dhamira yetu
ya kuwainua vijana na kuhakikisha
mpango huu wa Airtel FURSA unaleta tija na kuinua biashara zao.
Watakaoshiriki ni zaidi ya wafanyabiashara 28 na vikundi vinne
vilivyonufaika kwa kupatiwa vitendea kazi kupitia mradi wetu wa Airtel
FURSA ambao kwa sasa wanafanya vizuri katika biashara zao”.
Airtel
tumeona ni vyema tukiendelea kuwawezesha kwa kuwatafutia masoko
endelevu ndani na nje ya nchi kwa kuwashirikisha katika maonyesho haya
yenye lengo la kutangaza biashara zao
na kupata masoko zaidi, tunatoa wito kwa watanzania kuwaunga mkono kwa
kufatilia kazi zao kupitia mitandao ya kijamii na kupata fursa ya
kutembelea maonyesho haya siku ya kesho.
Bidhaa
zitakazo kuwepo katika maonyesho hayo ni pamoja na Sanaa za picha za
ukutani, vifaa vya magari, vyakula mbalimbali kama matunda ,korosho,
cake, mifugo kama vile kuku wa kisasa,
bidhaa za kiafrika, mapambo ya nyumbani na kadhalika.
0 comments:
Post a Comment