Mkurugenzi
Mkuu wa SBL Helene Weesie akiongoza katika kuzindua chapa mpya ya
Serengeti Premium Lager sherehe ambazo zinaambatana na maadhimisho ya
miaka 20 ya bia hiyo kulia kwake ni Meneja Masoko wa SBL Anitha na
kushoto kwake wa kwanza ni Mpishi Mkuu wa kwanza wa Serengeti Premium
Lager Winston kagusa na mwishoni ni Mkurungezi wa Masoko Cesear Mloka.Hafla hii ilifanyika katika hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi
Mkuu wa SBL Helene Weesie akizungumza na waandishi wa habari katika
mkutano na waandishi wa habari ambapo alitangaza maadhimisho ya miaka
20
tangu kuanzishwa kwa bia ya Serengeti Premium Lager (SPL) mwaka 1996.
Anayefuatia ni Meneja masoko wa SBL Anitha Msangi na kulia mwishoni ni
Mkurungezi wa Masoko wa SBL , Cesear Mloka .Mkutano huu umefanyika mapema leo katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es salaam
Mpishi Mkuu mtanzania Winston Kagusa aliyefanikiwa kuchanganya
mbinu ya utengenezaji wa bia za kijerumani na vionjo vya hapa nchini
kupata kinywaji hiki cha Serengeti Premium Lager kinachopendwa na
wengi.
Mkurugenzi
wa
Mawasiliano, SBL John Wanyacha akifafanua jambo kwa waandishi wa habari
katika Mkutano wa waandishi wa habari ambapo Bia ya serengeti premium
lager inatimiza miaka 20 toka kuanzishwa kwake na pia kuzinduliwa kwa
chapa yenye muonekano mpya.Mkutano huu ulifanyika mapema leo katika
hotel ya Hyatt Regency. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Waandishi wa habari wakichukua matukio katika mkutano huo uliofanyika mapema leo
Mkurungezi wa Masoko wa SBL , Cesear Mloka akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mara baada ya kutangazwa kwa maadhimisho ya miaka 20
tangu kuanzishwa kwa bia ya Serengeti Premium Lager (SPL) mwaka
1996.Anayefuatia katikati ni Meneja Masoko wa SBL Anitha Msangi na
mwishoni kulia ni Mkurungezi mkuu wa SBL Helene Weesie.Mkutano huu umefanyika mapema leo katika Hyatt Regency Hotel Jijini Dar es salaam.
************************
Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) leo imetangaza
kuanza kwa sherehe maalumu kuadhimisha miaka 20 tangu kuanzishwa
kwa bia ya Serengeti Premium Lager (SPL) mwaka 1996. Sherehe hizo zinaambatana
na uzinduzi upya wa bia hiyo ikiwa katika muonekano mpya.
Akizungumza leo
jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mkuu wa
SBL Helene Weesie, amesema mbali na kuonesha mafanikio ya bia ya Serengeti kwa
kipindi cha miongo miwilil iliyopita, kampuni ya SBL itatumia kipindi hiki kuwashukuru
wateja wake na umma wa Watanzania kwa kuikubali bia ya
Serengeti kama chaguo lao la hivyo kuifanya kuwa mingoni mwa bia zinazoongoza
hapa nchini.
“Tunawashukuru wateja
wetu, wafanya biashara, wasambazaji, mashirika ya sekta binafsi, serikali na
wadau wote ambao kimsingi wametusaidia na kuwa
nasi katika safari yetu hii ya mafaniko,” amesema Weesie.
Bia ya Serengeti Premium
Lager ni ya kwanza kutengenezwa kwa kimea kwa asilimia 100hapa nchini ikiwa
ni ubunifu wa Mpishi Mkuu mtanzania aitwaye Winston Kagusa ambaye
alichanganya mbinu ya utengenezaji wa bia za kijerumani na vionjo
vya hapa nchinikupata kupata kinwaji hiki kinacopendwa na wengi.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi
Mkuu, bia ya Serengeti ilizalishwa kwa mara ya kwanza ikilenga kufikia sehemu
ndogo maalumu ya soko lakini azma hii ilibadilishwa na kuzalishwa kwa wingi
kutokana na ongezeko kubwa la mahitaji ya bidhaa hiyo jambo ambalo
lilisababisha kuanzishwa uzalishaji zaidi katika viwanda vya SBL vilivyoko
Moshi na Mwanza.
Aidha Mkurugenzi huyo
ameendelea kusema kwamba katika kipindi chote cha miongo miwili bia ya
Serengeti imekuwa na vifungashio vya muonekano tofauti tofauti vinavyoakisi
mabadiliko ya kinyakati na mahitaji ya wateja wake. “muonekano mpya
tunaouzindua leo hii ni muendelezo wa kielelezo hiki kwamba daima SBL tunajali
mahitaji ya wateja wetu na tuko karibu nao, amesema Weesie.
“Tunaona fahari
kuzalisha Bia ya Serengeti Premium Lager katika ubora
uleule wa hali ya juu katika viwanda vyote vitatu, na huu ni uthibitisho halisi
kutokana na kutambuliwa na wateja wetu wa ndani pamoja na
medali zaidi ya 10 za kutambulika
kimataifa ambazo bia hii imeshinda. Tunaahidi wateja wetu kwamba
tutaendeleakuzalisha Serengeti Premium Lager katika ubora wa hali ya
juu kwa kuzingatia vigezo vya ubora vilivyoanishwa na Shirika la
Viwango Tanzania (TBS) na Shirika la Viwango la Kimataifa (ISO),” amesema
Weesie.
Uzinduzi wa muonekano
mpya wa bia ya Serengeti pia umekuja na
kauli mbiu mpya wa kinywaji hicho cha “Taifa Letu. Fahari Yetu. Bia Yetu.”
Aidha kampuni hiyo imewakaribisha wateja wake na wadau mbalimbali kutoka sekta
za umma na binafsi katika hafla ya maadhimisho ya miaka 20 ya bia ya Serengeti
yatakayofanyika leo jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment