Nafasi Ya Matangazo

October 21, 2016

Afisa wa Mpango wa Taifa wa kudhibiti Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Oscar Kaitaba akionesha waandishi wa habari kingatiba za Mabusha, Matende na Minyoo ambazo zitaanza kunywewa kuanzia Oktoba 25 hadi 30 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
*********

WANANCHI mkoani Dar es Salaam wanataraji kuanza kumeza  kingatiba ya mabusha, matende na minyoo kuanzia Oktoba 25- 30, mwaka huu.

Mratibu wa kitaifa wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele (NTDs), Dk Upendo Mwingira alisema kuwa watu wote wenye umri kuanzia miaka mitano na kuendelea watatakiwa kumeza dawa hizo.

Mwingira alisema kuwa dawa hizo hazina madhara yeyote kwa binadamu kama ambavyo mara kwa mara imekuwa ikielezwa hivyo amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kumeza dawa hizo ili kujikinga na magonjwa hayo ya Mabusha, Matende na minyoo ambayo huathiri ini na ubongo.

“ Dawa hizi hazina madhara kabisa, mamlaka husika ya ukaguzi wa chakula na dawa (TFDA) imeshazikakua  na kuzithibitisha, hivyo wananchi kuanzia umri wa miaka mitano na kuendelea wajitokeze kwa wingi kumeza dawa hizi katika vituo vya afya, na watoa huduma za dawa katika maeneo mbalimbali ya jijini Dar es Salaam zitakapokuwa zikitolewa,” alisema Dk Mwingira.

Alisema kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ndiye atakae zindua umezaji dawa huo katika kituo cha afya Buguruni hiyo Oktoba 25.
Wataalam hao wa afya wameiondoa hofu juu ya dawa hizo za kingatiba kuwa na madhara na kusema kuwa hazina madhara na hata wale wanaotumia kilevi wanaweza kuzimeza na baada ya saa mbili au tatu wakaweza kukata maji kama kawaida.
Wanahabari wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokluwa zikitolewa katika saemina hiyo ya siku moja iliyoandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na wawezeshaji kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) 

 Mwandishi wa BBC, Halima Kassim akifuatilia kwa makini mada ya Usubi.BOFYA HAPA KUONA ZAIDI.

Wanahabari wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokluwa zikitolewa katika saemina hiyo ya siku moja iliyoandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na wawezeshaji kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) 
Afisa wa Mpango wa Taifa wa kudhibiti Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Oscar Kaitaba akiendesha semina hiyo.
Afisa wa Mpango wa Taifa wa kudhibiti Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Oscar Kaitaba akionesha vifaa vya kupimia urefu kwaajili ya utoaji wa dawa hizo za kingatiba.
Wanahabari wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokluwa zikitolewa katika saemina hiyo ya siku moja iliyoandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na wawezeshaji kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) 
Afisa wa Mpango wa Taifa wa kudhibiti Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kutoka Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Oscar Kaitaba akiwapa dawa za kingatiba za Mabusha, Matende na Minyoo waandishi wa Habari Dar es salaam jana ambapo umezaji dawa huo kimkoa unataraji kufanyika kwa siku tano kuanzia Oktoba 25 hadi 30 mwaka huu.

 Dawa za kingatiba za minyoo
Dawa za kingatiba za Mabusha na Matende 
Miongoni mwa magonjwa ambayo yalikuwa hayapewi kipaumbele nchini ni pamoja na:- 

oUsubi - Onchocerciasis (river blindness)

oMatende na Mabusha - Lymphatic Filariasis

oTrakoma/Vikope - Trachoma

oKichocho - Schistosomiasis

oMinyoo ya Tumbo - Soil Transmitted Helminthiasis (Trichuris, Hookworm, Ascaris)

oMalale - Human African Trypanosomiasis

oKichaa cha Mbwa- Rabies

oTegu - Echinococcosis

oTegu - Cysticercosis

oBrucellosis

oTauni - Plague
Posted by MROKI On Friday, October 21, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo