Afisa wa Mpango wa Taifa wa kudhibiti Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Oscar Kaitaba akionesha waandishi wa habari kingatiba za Mabusha, Matende na Minyoo ambazo zitaanza kunywewa kuanzia Oktoba 25 hadi 30 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
*********
WANANCHI mkoani Dar es Salaam wanataraji
kuanza kumeza kingatiba ya mabusha,
matende na minyoo kuanzia Oktoba 25- 30, mwaka huu.
Mratibu wa kitaifa wa magonjwa
yaliyokuwa hayapewi kipaumbele (NTDs), Dk Upendo Mwingira alisema kuwa watu
wote wenye umri kuanzia miaka mitano na kuendelea watatakiwa kumeza dawa hizo.
Mwingira alisema kuwa dawa hizo hazina
madhara yeyote kwa binadamu kama ambavyo mara kwa mara imekuwa ikielezwa hivyo
amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kumeza dawa hizo ili kujikinga na
magonjwa hayo ya Mabusha, Matende na minyoo ambayo huathiri ini na ubongo.
“ Dawa hizi hazina madhara kabisa,
mamlaka husika ya ukaguzi wa chakula na dawa (TFDA) imeshazikakua na kuzithibitisha, hivyo wananchi kuanzia
umri wa miaka mitano na kuendelea wajitokeze kwa wingi kumeza dawa hizi katika
vituo vya afya, na watoa huduma za dawa katika maeneo mbalimbali ya jijini Dar
es Salaam zitakapokuwa zikitolewa,” alisema Dk Mwingira.
Alisema kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam ndiye atakae zindua umezaji dawa huo katika kituo cha afya Buguruni hiyo
Oktoba 25.
Wataalam hao wa afya wameiondoa hofu juu ya dawa hizo za kingatiba kuwa na madhara na kusema kuwa hazina madhara na hata wale wanaotumia kilevi wanaweza kuzimeza na baada ya saa mbili au tatu wakaweza kukata maji kama kawaida.
Wanahabari
wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokluwa zikitolewa katika
saemina hiyo ya siku moja iliyoandaliwa na Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na wawezeshaji kutoka
Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR)
Wanahabari wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokluwa zikitolewa katika saemina hiyo ya siku moja iliyoandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na wawezeshaji kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR)
Mwandishi wa BBC, Halima Kassim akifuatilia kwa makini mada ya Usubi.BOFYA HAPA KUONA ZAIDI.
Wanahabari wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokluwa zikitolewa katika saemina hiyo ya siku moja iliyoandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na wawezeshaji kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR)
Afisa
wa Mpango wa Taifa wa kudhibiti Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele
kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR),
Oscar Kaitaba akiendesha semina hiyo.
Afisa
wa Mpango wa Taifa wa kudhibiti Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele
kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR),
Oscar Kaitaba akionesha vifaa vya kupimia urefu kwaajili ya utoaji wa dawa hizo za kingatiba.
Wanahabari wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokluwa zikitolewa katika saemina hiyo ya siku moja iliyoandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na wawezeshaji kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR)
Afisa wa Mpango wa Taifa wa kudhibiti Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kutoka Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Oscar Kaitaba akiwapa dawa za kingatiba za Mabusha, Matende na Minyoo waandishi wa Habari Dar es salaam jana ambapo umezaji dawa huo kimkoa unataraji kufanyika kwa siku tano kuanzia Oktoba 25 hadi 30 mwaka huu.

Dawa za kingatiba za minyoo
Dawa za kingatiba za Mabusha na Matende
Miongoni mwa magonjwa ambayo yalikuwa hayapewi kipaumbele nchini ni pamoja na:-
oUsubi - Onchocerciasis (river
blindness)
oMatende na Mabusha - Lymphatic
Filariasis
oTrakoma/Vikope - Trachoma
oKichocho - Schistosomiasis
oMinyoo ya Tumbo - Soil Transmitted
Helminthiasis (Trichuris, Hookworm, Ascaris)
oMalale - Human African Trypanosomiasis
oKichaa cha Mbwa- Rabies
oTegu - Echinococcosis
oTegu - Cysticercosis
oBrucellosis
oTauni - Plague
No comments:
Post a Comment