Meneja
Mahusiano kwa Umma benki ya Posta Tanzania (TPB) Noves Moses
akizungumza katika hafla ya Makabidhiano ya mradi wa vyoo vya walimu
vyenye matundu matano katika shule ya Msingi Ipinda Wilayani Kyela
Mkoani Mbeya ambavyo ujenzi wake umeghalimu kiasi cha shilingi milioni
8kwa msaada wa benki hiyo ya Posta Tanzania.
Baadhi
ya wananchi,walimu na wazazi pamoja na wanafunzi shule ya Msingi Ipinda
Wilayani Kyela Mkoani Mbeya waliohudhuria hafla ya makabidhiano ya vyoo
vya walimu vilivyo jengwa kwa msaada wa benki ya Posta Tanzania TPB.
Wanafunzi
wa Shule ya Msingi Ipinda Wilayani kyela Mkoani Mbeya wakitoa burudani
katika hafla ya makabidhiano ya vyoo vya walimu vyenye matundu matano
ambavyo vimejengwa kwa msaada wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) kwa
thamani ya shilingi milioni 8.
Mwalimu
Mkuu wa Shule ya Msingi Ipinda Subira Gwakabale akishukuru kwa kupatiwa
msaada na benki ya Posta Tanzania (TPB) kwa kujengewa vyoo vya walimu
vyenye matundu 5 kwa thamani ya shilingi milioni 8 ,ambapo pia katika
katika shukrani zake ameelezea changamoto mbalimbali walizonazo ikiwa ni
pamoja na Idadi kubwa ya wananfunzi kuliko vyumba vya madarasa walivyo
navyo ambapo kwa sasa wana jumla ya wanafunzi 948 huku vyumba vya vya
madarasa vikiwa 8 tu hali ambayo inawawia vigumu katika utoaji wa huduma
kwa wanafunzi hao.
Meneja
wa Benki ya Posta Tanzania Tawi la Mbeya ,Humphrey Julias akizungumza
katika hafla hiyo ya makabidhiano ya vyoo vya walimu vyenye matundu
matano ambavyo vimejengwa na benki hiyo katika shule ya Msingi Ipinda
Wilayani Kyela. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Afisa
Taaluma Wilaya ya Kyela Lucasian Kavishe akiwaasa wananchi
waliohudhuria hafla ya makabidhiano ya vyoo vya walimu vilivyojengwa
katika Shule ya Msingi Ipinda kwa Msaada wa Benki ya Posta Tanzania
(TPB)kwa kuhakikisha wanatoa ushirikiano kwa wadau mbalimbali
wanaojitolea katika miradi mbalimbali ya kusaidia sekta ya elimu ili
kuendelea kuwapa moyo zaidi wa kusaidia
Meneja
wa benki ya Posta Tanzania (TPB)Mkoa wa Mbeya kulia ,Humphrey Julias
akiteta jambo na Meneja Mahusiano kwa Umma wa benki hiyo Noves Moses
kabla ya kukabidhi rasmi mradi wa vyoo vya walimu vyenye matundu matano
vilivyojengwa katika shule ya Msingi Ipinda Wilayani Kyela Mkoani Mbeya
kwa Msaada wa benki hiyo kwa thamani ya shilingi milioni 8.
Meneja
Mahusiano kwa Umma wa benki ya Posta Tanzania TPB,Noves Moses akizindua
na kukabidhi rasmi mradi wa vyoo vya walimu vyenye matundu Matano
ujenzi ambao umeghalimu kiasi cha shilingi milioni8 katika shule ya
Msingi Ipinda Wilayani kyela Mkoani Mbeya Otobar 13 mwaka huu,kushoto ni
mwenyekiti wa kijiji cha Ipinda Saadat Sam (katikati)Afisa elimu
taaluma Lucasian Kavishe na mwalimu Mkuu wa shule hiyo Subira Gwakabale
kulia .
Muonekano
wa jengo la vyoo vya walimu katika shule ya Msingi Ipinda lenye matundu
matano ambalo ujenzi wake umegharimu kiasi cha shilingi milioni8.
Meza kuu katika Picha ya pamoja na walimu na wajumbe wa bodi ya shule ya Msingi Pinda. |
Meza kuu na wafanyakazi wa benki ya Posta Tanzania TPB tawi la Kyela na Mbeya. |
Meza kuu katika picha ya pamoja na wadau na viongozi wa serikali ya kijiji cha Ipinda Wilaya ya Kyela. |
Vyoo vilivyokuwa vikitumiwa na walimu wa shule ya Msingi Ipinda kabla ya kujengewa vyoo vipya na benki ya Posta Tanzania (TPB).PICHA E.MADAFA |
0 comments:
Post a Comment