Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia
Suluhu Hassan akitembelea kiwanda cha kuchakata gesi cha Madimba mkoani Mtwara.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia
Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Kiwanda cha kuchakata gesi
cha Madimba Mhandisi.Leonce namna gesi inavyopokelewa na kuchakatwa na
kusafirishwa kwa watumiaji.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia
Suluhu Hassan akiangalia mfumo wa uendeshaji na usalama wa kiwanda cha
kuchakata gesi cha Madimba mkoani Mtwara.
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya
pamoja na viongozi na wafanyakazi wa kiwanda cha kuchakata gesi cha Madimba
mkoani Mtwara.
*************
Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amewataka wafanyakazi wa
kiwanda cha kuchakata gesi asilia kilichopo Madimba mkoani Mtwara wawe
wazalendo na wafanye kazi kwa bidii katika kulinda na kuutunza uwekezaji huo
mkubwa ambao serikali inautegemea katika uzalishaji wa nishati ya umeme wakati
taifa linaelekea kwenye nchi ya viwanda.
Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wafanyakazi na
watendaji wa kiwanda hicho baada ya kutembelea kiwanda kwa mara ya kwanza tangu
ashike wadhifa huo kwa lengo la kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa
kiwandani hapo akiwa katika ziara yake ya kikazi ya siku nne mkoani Mtwara.
Amesema kiwanda cha kuchakata gesi asilia ni hazina kubwa kwa
Taifa hivyo ni kikalindwa na kutunzwa ipasavyo kutokana na umuhimu wake katika
uzalishaji wa nishati ya umeme kwa maendeleo ya nchi.
Makamu wa Rais pia amewashukuru na kuwapongeza wafanyakazi wa kiwanda
hicho cha kuchakata gesi asilia cha Madimba na amewahakikishia kuwa serikali
itaendelea kuwajali na kuwathamini katika utendaji wao wa kazi na kwamba
serikali itahakikisha wafanyakazi wa kiwanda hicho wanapewa motisha ya kutosha
ili waongeze maradufu utendaji wao wa kazi ili malengo ya serikali ya kuleta
maendeleo kwa wananchi kupitia viwanda inatimia kwa sababu taifa litakuwa na
nishati ya umeme ya uhakika.
Makamu wa Rais amewataka watendaji wa Shirika la Maendeleo la Petroli
(TPDC) ambalo linasimamia mradi huo kuhakikisha wanatenga fedha kwa ajili ya
kusaidia huduma za jamii katika vijiji vinavyozunguka mradi huo kila mwaka ili
wananchi waweze kuwa walinzi wa mitambo hiyo.
Akitoa maelezo mafupi ya mradi huo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini Prof. James Mdoe amesema kiwanda hicho kina uwezo wa
kuchakata gesi ya futi za ujazo milioni 210 kwa siku.
0 comments:
Post a Comment