Waziri Mkuu Mh.Kassim Majaliwa akipokea msaada wa mil 16 kutoka kwa mmoja wa Waratibu wa majukwaa ya Wasap ya Leaders Furum na Uongozi Dr Ave Marie Semakafu (kulia) huku Waratibu wengine wakishuhudia ambao ni Benjamin Thompson Kasenyenda (wa tatu kushoto) na Belarus Nyasebwa (wa pili kulia).Kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu.
Wanachama wa magrupu mawili ya wasap(whatsapp), leo(Septemba 22) wamemkabidhi Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa, jumla ya 16m/-, kwa ajili kusaidia waathirika wa tetemeko mkoani Kagera.
Akiongea katika hafla hiyo,mmoja wa waratibu wa magrupu hayo Dk.Ave Marie Semakafu amesema fedha hizo ni michango ya wanachama wa magrupu hayo, yaitwayo The Leaders Forum na Jukwaa la Uongozi.
Amesema wanachama hao wameguswa na yaliyowakuta watanzania wenzao mkoani Kagera, hivyo,waliona njia pekee ya kuungana nao katika majonzi ya janga hilo ni kutoa kidogo wali nacho.
Dk Semakafu amewaasa watanzania wengine, hasa walioko kwenye vikundi mbalimbali hususani vya mitandaoni, kushiriki zoezi la kuwachangia waathirika hao kwa vyovyote wawezavyo, maana hali bado ni mbaya mkoani Kagera.Alisema madhumuni ya magrupu hayo ni kujadili maendeleo ya taifa pamoja na kutoa ushauri mbinu mvadala kuifikia ndoto ya Tanzania tunayoiyaka.
Tetemeko hilo lilitokea Septemba 10, ambapo watu 17 wamepoteza maisha,wengine zaidi ya 200 wameruhiwa,huku nyumba zaidi ya 800 zikiwa zimeharibika,zingine kuanguka. Akiongea katika hafla hiyo Waziri Mkuu aliwashukuru wanachama wa majukwa hayo akisema wanapaswa hafla kuigwa na makundi mengine nchini.
"Sisi kama serikali tunawashuru sana kwa moyo huo wa upendo kwa wenzetu wa Kagera,na hatutaishia hapa bali tutafanya hivyo kwa maandishi.
" Aliwahakikishia wachangiaji waliokabidhi misaada yao leo yakiwemo makampuni mbalimbali na vikundi vingine vitano kuwa atahakikisha misaada yote itawafikia walengwa.Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika ofisini kwa Waziri Mkuu Jijini Dar es Salaam.
Wanachama wa majukwaa hayo ni watu wa kada mbalimbali hususani viongozi wa serikali wa sasa na wastaafu,akiwemo Waziri Mkuu Mstaafu Mh.Mizengo Pinda.Wengine ni Mwaziri,Wabunge, wakuu wa mashirika ya umma na binafsi, wanataaluma wa vyuo vikuu,wanahabari, Wafanyabiashara na Viongozi wa vyama vya Siasa.
Waratibu wengine wa magrupu hayo ni Dereck Murusuli,Benjamin Thompson Kasenyenda,Leila Sheikh,Dr.Michael Francis,Maggid Mjengwa, Mustafa Ismail Kambona, Zamaradi Kawawa na June Warioba.
No comments:
Post a Comment