Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Col Martin Mkisi, akifungua Kikao kazi cha Kudhibiti Utumikishwaji wa watoto.
Col Mkisi, akishiriki ktk kikao kazi na wadau wengine.
Mkuu wa Wilaya Col Mkisi ktk picha ya pamoja na washiriki ktk kikao kazi cha Kudhibiti Utumikishwaji wa Watoto.
*****************
Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Col Martin Mkisi amefungua na kushiriki katika kikao kazi cha kubuni mikakati na usimamizi wa utekelezaji wa sheria za kudhibiti tatizo sugu wilayani hapa la utumikishwaji wa watoto.
Mpango huo umeshirikisha watekelezaji wa sheria Wilayani( Law enforcers) kama vile: watendaji ofisi ya mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi wa Halmashauri, Wakuu wa Idara, Mahakimu, polisi,Usalama na Maafisa Magereza.
Mpango huo unaofadhiriwa na WEKEZA chini ufadhiri wa USAID,pamoja na mambo mengine, unalenga katika kupinga utumikishwaji wa watoto, ajira za watoto, utoroshaji wa watoto kwenda kufanya kazi hatarishi na mimba za utotoni, katika mikoa ya Tanga na Kigoma.
Aidha,Washiriki ktk mpango huo, wameondoka na azimio la kwenda kukomesha tatizo hili sugu hasa ktk kata za Kagerankanda, Heru -Ushingo, Kitagata na Nyamidaho Wilayani Kasulu.
No comments:
Post a Comment