Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.
Anastazia Wambura akiongea na wanamichezo na wadau wa michezo katika hafla ya kuwaaga wanamichezo wanaokwenda
kuiwakilisha Tanzania nchini Brazil katika
mashindano ya Olimpiki kwa mwaka 2016 leo Agosti 1, 2016.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni sanaa na
Michezo Mhe. Anastazia Wambura( katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja
na wanamichezo waliowahi kushiriki mashindano ya Olimpiki leo Agosti 1, 2016 kulia waliokaa ni Katibu
Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.
Anastazia Wambura akiongea na wanamichezo na wadau wa michezo katika hafla ya kuwaaga wanamichezo wanaokwenda
kuiwakilisha Tanzania nchini Brazil katika
mashindano ya Olimpiki kwa mwaka 2016 leo Agosti 1, 2016.
Picha/Habari na Raymond Mushumbusi
Serikali
imewashukuru wadau wa michezo nchini kwa kujitokeza na kuwa mstari wa mbele kushiriki
na kudhamini michezo mbalimbali nchini.
Shukrani
hizo zimetolewa leo na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.
Anastazia Wambura alipokuwa akizungumza na wanamichezo wanaokwenda kushiriki mashindano
ya Olimpiki kwa mwaka 2016 yanayofanyika Jijini Rio dejaneiro nchini Brazil.
Mhe.
Anastazia Wambura amesema kuwa wadau wa michezo wamekuwa wakishirikiana na
Serikali sio katika suala la michezo pekee hata katika habari na Sanaa na
amewapongeza kampuni ya ving’amuzi ya Multichoice Tanzania (DSTV) na Bodi ya Utalii
katika azma yao ya kuunga mkono maendeleo ya sera ya michezo nchini.
“Napenda
kuwashukuru wadau wetu Dstv na Bodi ya Utalii, nawapongeza kwa kuona fursa hii
muhimu na kuitumia kuwatia moyo wawakilishi wa nchi yetu katika michezo ya Olimpiki
kwa mwaka 2016 mueendelee kuiunga mkono Serikali katika kutekeleza sera ya
maendeleo ya Michezo ili kufikia malengo” alisema Mhe. Anastazia.
Aidha
amewataka wawakilishi wa Olimpiki kutumia fursa hii ya wadau wa michezo waliojitokeza
kuwaunga mkono ikiwemo Bodi ya Utalii kutangaza utalii wa Tanzania kwa mataifa mengine watakayo kutana nayo katika mashindano
ya Olimpiki nchini Brazil.
Kwa
upande wake Mkurungezi Mkuu wa Multichoice Tanzania Bw.Maharage Chande
ameishukuru Serikali kwa kuwapa fursa ya kushirikiana na timu ya Olimpiki
kuitangaza michezo na kuitangaza Tanzania kimataifa na kuahidi kuendelea kushirikiana
na Serikali katika kuendeleza michezo nchini.
0 comments:
Post a Comment