Naibu
Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa(Tamisemi)Suleimani
Jaffo akizungumza wakati akifungua mafunzo ya kusimamia na kutumia mitambo na
magari ya kisasa ya kukusanya Taka ngumu kwenye majiji na halmashauri zilizopo
kwenye mpango wa kuendeleza miji kimkakati unaosimamiwa na Ofisi ya Rais kwa
mkopo kutoka Benki ya Dunia,kushoto ni Mratibu wa Mradi huo,Mhandisi Davis
Shemangale na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Arusha,Mrisho Gambo.
Baadhi ya washiriki wa
mafunzo ya usimamizi miundombinu ya ukusanyaji Taka ngumu wakimsikiliza Naibu
Waziri,Suleimani Jaffo.
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa(Tamisemi)Suleimani
Jaffo(aliyevaa tai nyekundu) akiwa ujumbe ofisi yake na watumishi wa halmashauri ya Jiji la Arusha wakati
akikagua eneo lililotengwa kwaajili ya kuchomea taka ngumu lilipo Dampo Kuu
jijini humo katika mpango wa kuendeleza miji kimkakati unaosimamiwa na Ofisi ya
Rais .
Naibu
Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa(Tamisemi)Suleimani
Jaffo akikagua Dampo la Jiji la Arusha liliboreshwa miundombinu yake kulia kwake ni Mkuu wa wilaya ya
Arusha,Mrisho Gambo.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za
Mitaa (Tamisemi) Suleimani Jaffo akifafanua jambo kwa waandishi wa habari.
Sehemu ya
magari maalumu yatakayohusika kukusanya Taka ngumu kutoka mitaa mbalimbali ya
Jiji la Arusha. Naibu Waziri Jaffo alitaka mitambo hiyo itumike kwa
malengo yaliyokusudiwa na kufanyiwa matengenezo kila mara ili iwe endelevu na
kuongeza kuwa serikali imeshaweka mikakati ya miji yote kuwa misafi.
0 comments:
Post a Comment