Makamu wa Rais , Samia Suluhu Hassan
amewasili mjini Lindi mchana huu akitokea mkoa wa Dar es Salaam kwa njia ya
barabara ambapo hapo kesho anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha Sikukuu ya Wakulima Nanenane kitaifa kwenye
viwanja wa Ngongo katika Manispaa ya Lindi.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufunga maonyesho hayo ya
Nane nane hapo kesho kwa niaba ya Rais Dk John Pombe Magufuli.
Alipowasili ikulu ndogo mjini Lindi, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amepokelewa na Mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali na wa vyama vya
siasa.
Katika Msafara wake, Makamu wa Rais ameambatana na Waziri wa Kilimo,Maliasili,mifugo na uvuvi wa serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar Hamad Rashid.
No comments:
Post a Comment