Mkuu wa kitengo cha Internet
Airtel Gaurav Dhingra akionyesha simu zinazopatikana kwenye maduka yote ya
Airtel katika ofa iliyozinduliwa hivi karibuni kufuatia tamko la serekali la
kuzima simu zote bandia ifikapo tarehe 16 Juni 2016. Simu hizo zinauzwa kwa
gharama nafuu kabisa.
**************
KUFUATIA tamko la serikali la
kuzima simu zote bandia ifikapo tarehe 16 Juni 2016, Airtel Tanzania imeanzisha
ofa kabambe ya “simu za bure na halisi" zinazopatikana katika maduka yote
ya Airtel.
Tangazo hilo limesema kwamba simu za Bure na halisi zinapataikana
kwa wateja wote wenye simu bandia na ambazo sio za viwango
vinavyokubalika katika soko la Tanzania , kwa kununua kifurushi
chenye dhamani ya sh. 22,000 / = Tshs tu. Simu hizi za bure
na halisi zinazotolewa na Airtel ikiwemo ITEL 2090 na FERO 180,
zikiwa na dakika 550 kwa kupiga mitandao yote, zenye ujumbe mfupi
3000 na 250 MB kwa muda wa miezi minne. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
Akitoa maoni yake juu ya ofa
hii, mkuu wa kitengo cha Internet Airtel Tanzania, Gaurav Dhingra alisema
"tunatambua kwamba baadhi ya wateja wetu bado wanatumia simu ambazo
hazina uhalisia, hivyo wako katika hatari ya kuzimiwa simu zao hapo itakapofika
siku ya Alhamisi, Juni 16. Kuwasaidia Wateja kuweza kununua simu zenye
kiwango kinachokubalika, tumeamua kutoa simu zenye uhalisi katika gharama nafuu
kabisa zenye vifurushi vitakavyoduma kwa muda wa miezi minne.
Kwa kuongezea, tuna simu za
aina tofauti tofauti ambazo ni smartphone kwa kuwapa wateja wetu uwezo wa
kuchagua zaidi kama vile Magnus Z11, Huawei Y3C na Techno W3 ambapo mteja
atapata kifurushi chenye dakika zaidi ya 1000. Hivyo basi , mteja wetu wa
Airtel mwenye simu iliyo bandia anatakiwa kufika kwenye duka letu lolote la
Airtel na simu yake ili aweze kununua simu yenye kiwango kinachokubalika.
"alinukuliwa Dhingra
Wateja wa Airtel wanaweza
kuhakikisha kama simu zao ni bandia au la, kupiga *#06# au kutembelea mawakala
katika maduka ya Airtel lililokaribu nae.
0 comments:
Post a Comment