Na
Geofrey Tengeneza
Bodi
ya Utalii Tanzania imeanzisha touvuti maalumu iitwayo Destination Tourism
Portal pamoja na nyenzo (App) kwa watumiaji wa simu za mikononi na hivyo
kuendelea kujikita zaidi katika matumizi ya tovuti na mitandao ya Kijamii
(e-marketing) katika kutekeleza majukumu yake ya utangazaji wa vivutio vya
Utalii vya Tanzania duniani kwa lengo la kuvutia watalii wengi zaidi.
“Tovuti
hii inalenga zaidi katika kuwasaidia wajasiriamali wadogo na wa kati katika
sekta ya utalii kufanya biashara zao kwa urahisi na kukuza mapato yao na faida
zaidi” alisema Bw. Chitaunga.
Ameongeza
kuwa Tovuti hii inatumia anuani ya www.tanzaniatourism.com ina taarifa nyingi
sana za
vivutio
vya utalii vinavyopatikana hapa nchini lakini pia taarifa kuhusu malazi
(accommodation) na huduma nyinginezo na kwamba inamwezesha mtalii kufanya
malipo online.
Mkurugenzi
huyo wa Masoko amesema kuwa sambamba na uanzishaji wa tovuti hiyo, tumeanzisha
pia nyenzo rasmi ya Utalii iitwayo Tanzania Tourism App ambayo kama ilivyo kwa
portal ina taarifa nyingi za utalii ikiwa ni pamoja na vivutio vya utalii,
malazi na namna ya kupanga safari kwa mtalii anayetaka kutembelea Tanzania, na
kufanya malipo online.
Amesema
kuwa Nyenzo (App) hii inapatikana katika Google play store kwa watumiaji wa
simu za Android duniani kote na muda si mrefu itapatikana pia katika AppStore
kwa watumiaji wa simu za Iphone.
Amedokea
kuwa zipo nyenzo (Apps) kadhaa zilizoanzishwa na makapuni au watu binafsi kama
vile Tanzania Safari Guide; Tanzania Travel Safari; Destination Tanzania:
Tanzania Travel and Tourism n.k lakini hii ya kwetu ndiyo hasa rasmi ya
Serikali.
0 comments:
Post a Comment