Mkuu wa Mkoa wa Lindi,Godfrey Zambi Akisoma
hotuba ya uzinduzi wa mradi wa PS3 mkoani Lindi, kwa ajili ya kuimarisha
mifumo ya Sekta ya Umma,Mh.Zambi alisema kuwa mradi huo utafanyika katika
mikoa 13, ambayo itaanza na mradi huo Lindi ikiwa ni mmoja wapo.
Kutoka Kushoto Ni Mkuu wa Wilaya ya
Ruangwa,Mariam Mtima,Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea,Pololeti Mgema na Mkuu wa
Wilaya ya Liwale Ephraim Mbaga Wakifuatilia kwa Umakini Hotuba ya Mkuu wa Mkoa
wa Lindi wakati wa Ufunguzi huo.
Conrad
Mbuya ,Mkurugenzi wa Shughuli za Mikoa PS3 akitoa maelezo Kwa
washiriki toka Halmashauri zote za Mkoa wa Lindi jinsi mradi utakavyo
fanya kazi na afua zitakazo zingatiwa katika kutekeleza mradi huo.
Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Sheria Ofisi ya
Rais TAMISEMI,Edwin Mgendera alipokuwa akitoa maelezo kuhusu jukumu la
TAMISEMI katika uzinduzi wa mradi wa PS3 mkoani Lindi, kwa ajili ya kuimarisha
mifumo ya Sekta ya Umma
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi
Akipokea Taarifa Fupi ya Mradi wa PS 3 Toka kwa Mshauri wa Habari na
Mawasiliano PS 3,Bi Leah Mwainyekule
Washiriki wa Uzinduzi huo kutoka Sekretarieti ya
Mkoa wa Lindi pamoja na washiriki toka katika Halmashauri 6 za Mkoa Huo wakiwa
katika Picha ya Pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Lindi(Mwenye suti ya bluu katikati
waliokaa)Mara baada ya Uzinduzi wa Mradi huo Mjini Lindi. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
*******************
KATIKA kuimarisha Ubora wa Utoaji huduma za Umma
na Matumizi yake kwa ajili ya Kuboresha na kuimarisha Mifumo,Mkoa wa Lindi
Umezindua Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya sekta za umma utakaowezesha Jamii
katika Ngazi ya halmashauri kutumia rasilimali kwa Uwazi na kuwezesha
ushirikishwaji wa wananchi katika kupanga na kufuatilia matokeo ya kila
sekta.
Mpango huo utakaosaidia utoaji wa ushauri wa
kitaalamu na kuwajengea uwezo wafanyakazi ili kuongeza Usawa wa mgawanyo
wa rasilimali watu kwa ajili ya utoaji huduma wa bora katika maeneo yenye
Uhitaji zaidi ikiwemo mfumo wa ajira pamoja na kudumisha watumishi katika Ajira
Serikalini
Akizindua Mradi huo wa PS 3,Mkuu wa Mkoa wa
Lindi Godfrey Zambi amesema kuwa mradi huo wa uhimarishwaji wa mifumo ya
sekta za Umma nchini utasaidia kuondoa tatizo sugu la watumishi hewa endapo
utekelezaji wake utafanyika vizuri.
Awali akitoa taarifa katika uzinduzi huo,
Mkurugenzi wa Mradi katika Mikoa, Dk.Conrad Mbuya alisema mradi huo
utahakikisha mifumo iliyopo katika ngazi ya Halmashauri inaimarishwa kupitia
kitita cha afua zilizoundwa kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa utoaji huduma kwa
wananchi wa Tanzania.
Kufuatia Uzinduzi wa Mradi huo,Mkuu wa Wilaya ya
Lindi Yahya Nawanda pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa Abuu
MjakA walieleza kuwa mradi huo pia utasaidia ongezeko la pato la ndani
kwa ajili ya huduma za umma ikiwemo ushirikishwaji wa Madiwani katika
Utekelezaji wa mradi huo Utakaoboresha Utendaji na Uwajibikaji katika kutoa
huduma kwa Jamii.
Mradi huo uliozinduliwa leo unatekelezwa katika
mikoa 13 ya Tanzania Bara ambayo ni Iringa, Dodoma, Kagera, Kigoma,Mara,Mbeya,
Morogoro, Mtwara,Mwanza, Njombe, Rukwa na Shinyanga pamoja na Lindi.
0 comments:
Post a Comment