Nafasi Ya Matangazo

June 03, 2016

 Mkuu wa Mkoa wa Lindi,Godfrey Zambi Akisoma hotuba ya uzinduzi  wa mradi wa PS3 mkoani Lindi, kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya Sekta ya Umma,Mh.Zambi  alisema kuwa mradi huo utafanyika katika mikoa 13, ambayo itaanza na mradi huo Lindi ikiwa  ni mmoja wapo.
Kutoka Kushoto Ni Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa,Mariam Mtima,Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea,Pololeti Mgema na Mkuu wa Wilaya ya Liwale Ephraim Mbaga Wakifuatilia kwa Umakini Hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi wakati wa Ufunguzi huo.
Conrad Mbuya ,Mkurugenzi wa Shughuli  za Mikoa PS3  akitoa maelezo Kwa washiriki toka Halmashauri zote za Mkoa wa  Lindi jinsi mradi utakavyo fanya kazi na afua zitakazo zingatiwa katika kutekeleza mradi huo.
Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Sheria Ofisi ya Rais TAMISEMI,Edwin Mgendera alipokuwa akitoa maelezo kuhusu jukumu la TAMISEMI katika uzinduzi wa mradi wa PS3 mkoani Lindi, kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya Sekta ya Umma
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi  Akipokea Taarifa Fupi ya Mradi wa PS 3 Toka kwa Mshauri wa Habari na Mawasiliano PS 3,Bi Leah Mwainyekule

Washiriki wa Uzinduzi huo kutoka Sekretarieti ya Mkoa wa Lindi pamoja na washiriki toka katika Halmashauri 6 za Mkoa Huo wakiwa katika Picha ya Pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Lindi(Mwenye suti ya bluu katikati waliokaa)Mara baada ya  Uzinduzi wa Mradi huo Mjini Lindi. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.

*******************

KATIKA kuimarisha Ubora wa Utoaji huduma za Umma na Matumizi yake kwa ajili ya Kuboresha na kuimarisha Mifumo,Mkoa wa Lindi Umezindua Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya sekta za umma utakaowezesha Jamii katika Ngazi ya halmashauri kutumia rasilimali kwa Uwazi na kuwezesha ushirikishwaji wa wananchi katika kupanga  na kufuatilia matokeo ya kila sekta.

Mpango huo utakaosaidia utoaji wa ushauri wa kitaalamu na kuwajengea uwezo wafanyakazi ili  kuongeza Usawa wa mgawanyo wa rasilimali watu kwa ajili ya utoaji huduma wa bora katika maeneo yenye Uhitaji zaidi ikiwemo mfumo wa ajira pamoja na kudumisha watumishi katika Ajira Serikalini

Akizindua Mradi huo wa PS 3,Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi amesema  kuwa mradi huo wa uhimarishwaji wa mifumo ya sekta za Umma nchini utasaidia kuondoa tatizo sugu la watumishi hewa endapo utekelezaji wake utafanyika vizuri.

Awali akitoa  taarifa katika uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Mradi katika Mikoa, Dk.Conrad Mbuya alisema mradi huo utahakikisha mifumo iliyopo katika ngazi ya Halmashauri inaimarishwa kupitia kitita cha afua zilizoundwa kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa utoaji huduma kwa wananchi wa Tanzania.

Kufuatia Uzinduzi wa Mradi huo,Mkuu wa Wilaya ya Lindi Yahya Nawanda pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa Abuu MjakA walieleza  kuwa mradi huo pia utasaidia ongezeko la pato la ndani kwa ajili ya huduma za umma ikiwemo ushirikishwaji wa Madiwani katika Utekelezaji wa mradi huo Utakaoboresha Utendaji na Uwajibikaji katika kutoa huduma kwa Jamii.

Mradi huo uliozinduliwa leo unatekelezwa katika mikoa 13 ya Tanzania Bara ambayo ni Iringa, Dodoma, Kagera, Kigoma,Mara,Mbeya, Morogoro, Mtwara,Mwanza, Njombe, Rukwa na Shinyanga pamoja na Lindi.


Posted by MROKI On Friday, June 03, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo