May 26, 2016

CHINA KUENDELEZA USHIRIKIANO NA SERIKALI YA TANZANIA KATIKA SEKTA ZA VIWANDA, NISHATI NA MIUNDOMBINU

Msemaji na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mindi Kasiga, akizungumza na waandishi wa habari juu ya ziara iliyofanywa nchini China na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk Aziz Malima, Mei 15-19 mwaka huu kufuatia mualiko wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China. Father Kidevu Blog inaandika zaidi. 
Kasiga, alisema serikali ya China imeahidi kuendeleza ushirikiano na serikali ya Tanzania katika nyanja ya uchumi kupitia uwekezaji kwenye sekta ya viwanda, nishati na miundombinu.

Dk Mlima alikutana na kufanya mazungumzo na  Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Zhang Ming lakini pia na viongozi wengine mbalimbali wa serikali pamoja na makampuni makubwa ya China ambayo yamewekeza nchini.

Pamoja na Mambo mengine yaliyojitokeza katika mazunguzo yao ni China kusisitiza dhamira yake ya dhati ya kukuza usrikiano na Tanzania katika nyanja ya uchumi kupitia uwekezaji kwemnye sekta ya viwanda, nishati na miundombinu.China imeweka kipaumbele cha juu katika miradi ya ujenzi wa bandari ya bagamoyo na eneo la viwanda pamoja na maboresho ya reli ya TAZARA na ipo tayari kuanza upembuzi yakinifu wa reli ya Kati. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.


Aidha katika ujenzi wa barandari ya Bagamoyo, Kampuni ya china ya Merchant Holding International (CMHI) ambayo imengia ubia na serikali ya Tanzania na mfuko wa Oman wapo katika hatua nzuri ya kukamilisha mazungumzo ya ubia wao.
Kasiga,aliwaambia wanahabari kuwa Katibu Mkuu Dk Malima, alikutana na Kamishna wa State tobacco Monopology, Lin Chengxing ambapo walizungumzia utekelezaji wa Mkataba wa Kuruhusu Tumbaku Ya Tanzania kuingia katika soko la China uliosainiwa mwaka 2013 wakati Rais wa nchi hiyo, Xi Jinping alipofanya ziara nchini na makampuni mawili ya China yamepewa jukumu la kununua tumbaku ya Tanzania.


Katika mkutano mwingine Dk Malima alikutana na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mambo ya nje cha China, Prof Qin Yaqing ambapo walikubaliana kuimarisha ushirikiano baina ya chuo hicho na chuo cha Diplomasia cha hapa nchini.

Wawili hao walikubaliana kushirikiano katika tafiti na utoaji wa mihadhara na chuo hicho kuahidi kutoa nafasi za masomo kwa wakufunzi wa Chuo cha Diplomasia na watumishi wa Wizara.

No comments:

Post a Comment