Mkurugenzi Mkuu
wa TBL Group ,Roberto Jarrin (kulia) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari , wakati lipokuwa akitoa
tathmini ya utendaji kazi wa kampuni hiyo kwa kipindi cha mwaka jana na
kutangaza mikakati ya mwaka huu. Mkutano
huo ulifanyika makao
makuu ya
kampuni hiyo Ilala
jijini Dar es Salaam leo Mei 26,2016.
Mwndishi wa
gazeti la The East Africa Kidanda Christopher akiuliza swali kwa Mkurugenzi
Mkuu wa TBL Group ,Roberto Jarrin (hayupo pichani) kuhusiana na uzalishaji wa pombe za asili , wakati wa
mkutno na wandishi wa habari wa kutoa tathmini ya utendaji kazi wa kampuni hiyo
kwa kipindi cha mwaka jana na kutangaza mikakati ya mwaka huu.
Baadhi y
waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali waliohudhuria katika mkutano wa
TBL Group , wa kutoa tathmini ya utendaji kazi wa kampuni hiyo kwa kipindi cha
mwaka jana na kutangaza mikakati ya mwaka huu,
wakimsikiza kwa makini, Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group ,Roberto Jarrin (hayupo
pichni) wakati wa mkutano huo ulifanyika makao makuu ya kampuni hiyo Ilala jijini Dar es
Salaam, leo Mei
26 2016.
Baadhi
ya wandishi wa habari wakitembelea maeneo ya uzalishji wa kiwanda cha TBL Ilala
jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa
habari kutoka vyombo mablimbali wakipata maelezo ya uzalishaji wa bia kutoka
kwa mmoja wa wafanyakazi wa TBL Group leo Mei 26,2016 . Wakati walipotembelea
kiwanda hicho.
Mtalamu wa upishi
wa vinywaji wa TBL Group (Techincal Brewer) Emanuel Sawa akiwaonyesha waandishi
wa habari moja ya bia aina ya Castle Luger, jinsi ianavyozalishwa wakati
wlipotembelea kiwand hicho mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa tathmini ya utendaji kazi wa kampuni hiyo kwa
kipindi cha mwaka jana na kutangaza mikakati ya mwaka huu, ulifanyika makao makuu ya kampuni hiyo Ilala jijini Dar es Salaam leo Mei
26,2016. BOFYA HAPA KWA TAARIFA ZAIDI.
************************
KAMPUNI
ya TBL Group imelipa kodi ya mapato ya kiasi cha shilingi bilioni 81 katika
kipindi cha mwaka 2015.
Akitoa taarifa
ya tathmini ya utendaji wa kampuni ya mwaka uliopita kwa waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam leo,Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group Roberto Jarrin pia
amebainisha kuwa mbali na kampuni kulipa kiasi hicho cha kodi pia imekusanya
kodi za serikali kiasi cha shilingi bilioni165 ikiwa ni kodi ya mlaji
(exercise duty) ,bilioni 114 ikiwa ni kodi ya ongezeko la thamani (VAT) na bilioni 24 ikiwa ni
malipo ya kodi nyinginezo ikiwemo kodi ya PAYE.
TBL Group ni kampuni inayoongoza kulipa kodi nchini ikiwa imechagia pato la
serikali kwa njia ya kodi kiasi cha shilingi Trilioni 2.3 katika kipindi cha
miaka 10 “Kampuni yetu imechangia maendeleo ya taifa kwa njia ya kukusanya na
kulipa kodi na mchango huo umekuwa ukitambuliwa na taasisi mbalimbali na
kuitunukia tuzo ikiwemo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambayo imeitunukia
tuzo ya Mlipa kodi bora nchini kwa kipindi cha miaka mine mfululizo”.Alisema
Jarrin.
TBL Group inajumuisha makampuni ya- Tanzania Breweries Limited (TBL), Tanzania Distilleries
Limited (TDL) na Dar Brew Limited.Biashara kuu ya
kampuni ni kuzalisha na kuuza vinywaji ikiwemo bia za aina mbalimbali,vinywaji
vikali na vinywaji vya asili..
Jarrin alibainisha hayo wakati akitoa ripoti ya utendaji wa kampuni
katika kipindi cha mwaka 2015 na mikakati yake ya mbele katika kipindi cha
mwaka 2016/17 kwa waandishi wa habari “TBL Group itaendelea kuunga jitihada za
serikali zakukuza sekta ya viwanda nchini kwa kuendelea kujenga viwanda nchini
na tangu kampuni hiyo ibinafsishwe mwaka 1994,imekuwa ikiendelea kuwekeza na
tayari imewekeza Zaidi ya shilingi bilioni 150 kwa ajili ya kujenga viwanda
vilivyokuwepo awali uwa vya kisasa Zaidi kuendana a teknolojia ya kisasa”
Kampuni inavyo viwanda 10 nchini na miongoni wa viwanda vyake vilivyopo
katika mikoa ya Mwanza,Mbeya na Dar es Salaam vimetunukiwa tuzo mfululizo za
kuwa viwanda bora katika viwanda vinavyomilikiwa a kampuni mama ya SABMiller
katika bara la Afrika.TBL Mwanza na Mbeya vikiwa katika kundi la viwanda 10 na
15 kwa ubora duniani.
Jarrin alisema biashara ya bia za kampuni ya TBL zinatawala soko kwa
asilimia 78 nchini ikiwa inaongozwa na aina za bia za Safari, Kilimanjaro, Ndovu, Castle lager na
Castle Lite .Pia kampuni
inatengeneza mvinyo
na vinywaji vikali maarufu vinavyotamba kwenye soko kwa asilimia 73 ambavyo
ni - Konyagi, Valuer and Dodoma Wine - Kwa upande wa vinywaji vya asili vinywaji vyake vinatawala soko kwa
asilimia 8 ambavyo ni – Chibuku
and Nzagamba - Utafiti uliofanywa na taasisi ya CanBack
kuhusiana na matumizi ya pombe za asili nchini umebainisha kuwa matumizi ya pombe za asili
nchini ni asilimia 50%
Jarrin aliendelea kueleza kuwa TBL Group inaendelea kutoa mchango
wa kukuza uchumi wa taifa kupitia katika sekta ya uuzaji vinywaji ambayo imetoa
ajira zaidi ya milioni 2 za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja
zinazoendelea kuwanufaisha watanzania wa kada mbalimbali.Kwa upande wa sekta ya
kilimo wakulima wa zao la Shahiri Zaidi ya 3000 wamenufaika kupitia mpango wa
kushirikiana na kampuni.Katika kipindi cha mwaka 2015 mpango huu umewezesha
ongezeko la uzalishaji wa zao hilo kufikia tani 15,574 kiasi ambacho kimevuka
lengo la matumizi na mahitaji ya kampuni.
Pia imebainishwa kuwa zaidi ya wakulima 700 wananufaika na mpango wa
kiwanda cha TDL wa kushirikiana nao atika kilimo cha zabibu kinachoendeshwa
katika vijiji vya Bihawana,
Mpunguzi,, Mvumi, Hombolo, Mbabala, Veyula, Makang’wa, Mzakwe na Mbalawala
.Chini ya mpango huo wakulima wanawezeshwa kupatiwa utaalamu wa kilimo kwa
kushirikiana na taasisi yaMakutupora Viticulture Training and Research Center
(MVTRC). Pia chini ya mpango huu watoto wa wakulima wa zao la zabibu wamekuwa
wakisaidiwa kielimu kupitia mfuko unaojulikana kama Zabibu na Shule Kwanza.
Jarrin pia alibainisha kuwa kampuni ya DarBrew imeweza kuleta mapinduzi
ya uuzaji wa pombe za asili nchini kwa kuwawezesha watumiaji kupata kinywaji
cha Chibuku na Nzagamba kikiwa kimefungwa kwa viwango mbalimbali na katika mazingira ya usafi yanayolinda afya
za watumiaji na hivi sasa imekuja na mkakati wa kuwainua akina mama kimapato
kupitia kuuza bidhaa zake unaojulikana kama Chibuku Mamas ambao hadi kufikia
sasa wanawake wapatao 130 wameishajiunga na mpango huu.
Kuhusu mtazamo wake wa hali ya biashara ya kampuni kwa sasa Jarrin
alisema sekta ya uuzaji wa vinywaji inakabiliwa na changamoto mbalimbali
mojawapo ni bei kubwa ya bia ambayo watumiaji wake wengi wanashindwa
kuimudu,kuwepo na vinywaji visivyo katika mfumo rasmi wa ushindani katika
soko,kukosekana kwa motisha katika uzalishaji wa malighafi za kutengeneza
vinywaji nchini kwa kuwa zinatozwa kodi kubwa ya zuio kuliko malighafi
zinazotolewa nje ya nchi.
Alisema baadhi ya mambo yanayostahili kufanyika katika uboreshaji wa
sekta ili iendelee kuchangia pato la taifa ni kupunguza kodi za malighafi zinazozalishwa nchini kama
kimea kinachotumika kutengeneza bia pia kulasimisha pombe za asili ziende sambamba na vinywaji vya sili
vinavyolipiwa kodi na kuhakikisha vinywaji vya asili vinapatikana katika mazingira ya usafi “Pamoja na changamoto nyingi zilizopo
katika sekta hii tunaendelea kukabiliana nazo na tumedhihirisha uwezo wetu kwa
kuwa na viwanda vyenye ubora wa hali ya juu nchini Tanzania”Alisema Jarrin.
No comments:
Post a Comment