October 04, 2015

STOP PRESS: MZEE KINGUNGE NGOMBARE MWIRU AJITOA RASMI CCM

Mwanasisa Mkongwe wa Chama cha Mapinduzi na aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali za chama na serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kingunge Ngombare Mwiru ametangaza rasmi hivi punde kujiengua ndani ya chama hicho.

Ngingunge amesema ameamua kufanya hivyo kutokana na kile alichoamini kuwa CCM haifanyi yale yaliyoasisiwa na kujengewa Misingi bora na waasisi wake. 

Aidha amesema hakusudii kujiunga na Chama Chochote cha Siasa nchini bali atakuwa mtanzania huru. 

Akizungumzia hali ya sasa kisiasa amesema kila kindi katika jamii hivi sasa linataka mabadiliko. 

Kingunge ametangaza uamuzi wake huo hivi pinde katika mkutano wake na waandishi wa habari ambao unarushwa moja kwa moja na kituo cha Televisheni cha ITV. 

4 comments:

  1. kila mtanzania ana haki ya kuamua kujiunga na kujiondoa ktk chama chochote cha kisiasa.mzee ni haki yake kuongea na kuamua anchokiona ni sahihi.
    lakini mimi nasikitishwa na suala la wewe mtoa posti kuona kama hilo ni la muhimu sana kwa mtanzania,taifa hili kwa sasa linamatatizo mengi ya dharula.kwanini hauweki posti zenye manufaa ktk taifa kama suala tahadhari juu ya ELMINO,BONDE LA UFA,KIPINDUPINDU,UCHOMWAJI WA NYUMBA ZA IBADA. NA PIA MSIBA WA MWANAHARAKI WA MAPINDUZI MCHUNGAJI MTIKIRA (R.I.P).
    Tumia vizuri karam yako ili kureta manufaa ya taifa
    BY Mophat michael mwanaharakati binafsi nisiefungamana na chama

    ReplyDelete
    Replies
    1. atatoa na posts hizo usihofu kimsingi mpaka azihakiki sio kukurupuka tu

      Delete
  2. Ndugu yangu uliyejitambulisha kwa jina la Mophat Michael
    sidhani kama unasoma na wala kama umsomaji mzuri wa blogu hii ya bwana Kidevu.

    Hii ni miongoni mwa Blogu ambazo binafis nikihitaji habari makini na uhakika huzipata humu.

    Hiyo ya kifo cha Mtikila mbona ipo humu tena imeandikwa vizuri zaidi. Hizo za elinino kama unazo uwe umantumia na sio jkutoa lawama tu. Jamali -Kasulu Kigoma

    ReplyDelete
  3. nazani mophat michael hujaisoma hii blog info zake

    ReplyDelete