Mtu mmoja amepoteza maisha papo hapo baada ya gari alilokua akitembelea Corola Primio lenye nambanza usajili T 444 CST kuangukiwa na Lori aina ya Scania T 424AEB lililo beba Kontena na kuvutwa na tela lenye namba za usajili T 653ABW ambalo lilipinduka hii leo mchana katika eneo la Temeke Vetenary jirani na soko barabara kuu ya Mandela, Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam. Mtu mmoja mwanamke alinusurika katika ajali hiyo baada ya kutoka salama na kutoweka. ©FK Blo
Wananchi wakiwa wamekusanyika wakiangalia uokoaji kutoka kwa kikosibcha zimamoto cha jiji la Dar es Salaam wakisaidiana na wananchi.
Gari hilo dogo likiwa limeharibika vibaya likisogezwa tayari kwa kukatwa na kutoa mwili wa marehemu.
Lori hilo likiwa limeanguka na kulaloa gari hilo dogo lililokua likitokea eneo la Tazara sambamba na lori hilo.
No comments:
Post a Comment