Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiitambulisha
chapa ya Bwana Sukari katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika Serena Hotel jiji
Dar es Salaam jana. Wanaongalia ni Balozi Ami Mpungwe,
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik, Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda
cha Sukari Kilombero Mark Bainbridge na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari
Tanzania Henry Semwanza.
Mkurugenzi wa Masoko wa
Kiwanda cha Sukari Kilombero Ephraim
Mafuru, akimfafanulia Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuhusu chapa ya mpya Bwana Sukari iliyozinduliwa jijini
Dar es Salaam jana. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akihutubia wakati wa uzinduzi
wa Chapa ya Bwana Sukari uliofanyika Serena Hotel jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Sukari Kilombero Mark Bainbridge,
akihutubia wakati wa uzinduzi wa Chapa ya Bwana Sukari katika hafla
iliyofanyika Serena Hotel jijini Dar es Salaam jana. Waziri Mkuu Mizengo Pinda
ndiye aliyefanya uzinduzi huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya
Sukari Tanzania, Henry Semwanza akihutubia wakati wa uzinduzi wa Chapa ya Bwana
Sukari iliyofanyika Serena Hoteli jijini Dar es Salaam jana. Waziri Mkuu
Mizengo Pinda ndiye aliyefanya uzinduzi huo. SOMA ZAIDI BOFYA HAPA
****************
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda ametoa pongezi kwa uongozi wa Kampuni ya
Kilombero Sugar kwa juhudi zao za kuwawezesha maelfu ya wakazi wa mkoa wa
Morogoro kubadili maisha yao kutokana na fursa wanazopatoa.
Pinda alitoa pongezi hizo wakati
wa hafla iliyofanyika katika hoteli ya Serena Jumanne jijini Dar es Salaam
wakati akizundua nembo mpya ya Bwana Sukari. “Kiwanda cha sukari cha Kilombero
ni chanzo cha uhakika cha ajira za watu 40,000 ambapo ni msaada mkubwa kwa zaidi
ya familia 80,000 zinazoishi wilaya ya
Kilombero na Kidatu. Hili ni jambo la kushukuriwa sana”, alisema Pinda.
Wakazi wa Kidatu na Kilombero
wamekuwa na uwezo wa kujenga makazi bora, kuendesha biashara zao ndogondogo, na
muhimu zaidi ni namna wanavyoweza kuwasomesha wato wao kutokana na kipato cha
uhakika kutoka Kilombero Sugar,” Waziri Mkuu aliimbia hadhira ambayo hiyo,
akiwemo Mkurugenzi wa Bodi ya Sukari
nchini Henry Semwaza.
Kiwanda hicho cha kuzalisha
sukari pia kinawapa fursa nzuri wakulima wadogo wa miwa mkoani humo kujipatia
kipato kinachowawezesha kuishi maisha yao ya kila siku. Katika mwaka wa fedha
uliopita, Kiwanda cha Sukari cha Kilombero kilinunua malighafi (miwa)
zilizogharimu kiasi cha shilingi bilioni 33.379 kutoka kwa wakulima wadogo
ikiwa ni ongezeko la asilimia 9.2 ikilinganishwa na kiasi kilicholipwa kwa
wakulima hao mwaka wa fedha uliotangulia.
Mahitaji ya sukari nchini ni
jumla ya tani 570,000 wakati viwanda vya ndani vina uwezo wa kuzalisha tani
320,000. “Ili kufidia pengo hilo serikali imekuwa ikitoa kibari kwa
wafanyabiashara kuagiza lakini baadhi yao wamekuwa si waminifu. Wanaagiza
sukari zaidi na kuingiza nchi kupitia njia za panya hivyo kuathiri wazalishaji
wa ndani”, alisema.
Pinda alisema serikali
inatambua juhudi zinazofanywa na kiwanda hicho kwa ajili ya maslahi ya jamii
inayoizunguka. “Hospitali mpya ambayo imejengwa hivi karibuni imekuwa ni msaada
mkubwa kwa wakazi wa Kidatu, Kilombero na maeneo ya jirani na hivyo kuepusha
adha ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya,” alisema.
Kiwanda cha Sukari cha
Kilombero kimewekeza zaidi ya shilingi milioni 700 kwa ajili ya ujenzi wa
hospitali ambayo kwa sasa inatoa huduma mbalimbali za afya kama vile X-ray,
upasuaji, uvimbe, afya ya mama mjamzito na
mototo mchanga.
Alisema Kiwanda cha Kilombero
ni miongoni mwa maeneo yanayolipa kodi kubwa sana nchini. “Katika mwaka wa
fedha uliopita, kiwanda cha Kilombero kichangia zaidi ya shilingi milioni 22
kwa serikali kupitia kodi mbalimbali.
Mapema katika hotuba yake ya
utambulisho, Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha cha Sukari cha Kilombero Bw. Mark
Bainbridge alielezea kuridhishwa kwake na sapoti kutoka kwa serikali na kuahidi
kuendelea kutoa bidhaa zenye ubora wa hali ya juu. “Kwa miaka zaidi ya
ishirini, Kiwanda cha Sukari kilombero
kimekuwa kikifanya biashara zake nchini kwa rekodi nzuri.
“Maamuzi yetu ya kuwa na muonekano
mpya wa Bwana Sukari yanatokana na utafiti wetu wa kina tuliofanya hivi
karibuni ambao umeoyesha kwamba sukari yetu inapendwa na Watanzania wengi
kutokana na u bora uliopo. Tunataka kuendeleza imani hii na kuthibitisha uwepo
na nia yetu kuendelea kuwa hapa na kulinda biashara yetu dhidi ya watu yenye
nia ya kuchafua jina la kampuni kwa wateja wetu,” alisema.
Alisema kampeni hii itatangazwa kupitia TV, radio, magazeti,
vyombo vya kidigitali na sampuli mbalimbali. “Lengo yetu ni kuhakikisha ujumbe
kuhusu sura mpya ya Bwana Sukari unawasilishwa vizuri na kueleweka vizuri kwa
kila mmoja,”alisema
Bidhaa ya Bwana Sukari imekuwa
ni maarufu sana katika mikoa ya Morogoro, Iringa, Mbeya, Dodoma na Dar es
Salaam ambako inauzwa sambamba na bidhaa nyingine.
No comments:
Post a Comment