Nafasi Ya Matangazo

October 22, 2015

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiitambulisha chapa ya Bwana Sukari katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika Serena Hotel jiji Dar es Salaam jana. Wanaongalia ni Balozi Ami Mpungwe, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik, Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Sukari Kilombero Mark Bainbridge na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania Henry Semwanza.

Mkurugenzi wa Masoko wa Kiwanda cha Sukari  Kilombero Ephraim Mafuru, akimfafanulia Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuhusu chapa  ya mpya Bwana Sukari iliyozinduliwa jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akihutubia wakati wa uzinduzi wa Chapa ya Bwana Sukari uliofanyika Serena Hotel jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Sukari Kilombero Mark Bainbridge, akihutubia wakati wa uzinduzi wa Chapa ya Bwana Sukari katika hafla iliyofanyika Serena Hotel jijini Dar es Salaam jana. Waziri Mkuu Mizengo Pinda ndiye aliyefanya uzinduzi huo.


Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania, Henry Semwanza akihutubia wakati wa uzinduzi wa Chapa ya Bwana Sukari iliyofanyika Serena Hoteli jijini Dar es Salaam jana. Waziri Mkuu Mizengo Pinda ndiye aliyefanya uzinduzi huo. SOMA ZAIDI BOFYA HAPA

****************
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda ametoa pongezi kwa uongozi wa Kampuni ya Kilombero Sugar kwa juhudi zao za kuwawezesha maelfu ya wakazi wa mkoa wa Morogoro kubadili maisha yao kutokana na fursa wanazopatoa.

Pinda alitoa pongezi hizo wakati wa hafla iliyofanyika katika hoteli ya Serena Jumanne jijini Dar es Salaam wakati akizundua nembo mpya ya Bwana Sukari. “Kiwanda cha sukari cha Kilombero ni chanzo cha uhakika cha ajira za watu 40,000 ambapo ni msaada mkubwa kwa zaidi ya  familia 80,000 zinazoishi wilaya ya Kilombero na Kidatu. Hili ni jambo la kushukuriwa sana”, alisema Pinda.  

Wakazi wa Kidatu na Kilombero wamekuwa na uwezo wa kujenga makazi bora, kuendesha biashara zao ndogondogo, na muhimu zaidi ni namna wanavyoweza kuwasomesha wato wao kutokana na kipato cha uhakika kutoka Kilombero Sugar,” Waziri Mkuu aliimbia hadhira ambayo hiyo, akiwemo Mkurugenzi  wa Bodi ya Sukari nchini Henry Semwaza.

Kiwanda hicho cha kuzalisha sukari pia kinawapa fursa nzuri wakulima wadogo wa miwa mkoani humo kujipatia kipato kinachowawezesha kuishi maisha yao ya kila siku. Katika mwaka wa fedha uliopita, Kiwanda cha Sukari cha Kilombero kilinunua malighafi (miwa) zilizogharimu kiasi cha shilingi bilioni 33.379 kutoka kwa wakulima wadogo ikiwa ni ongezeko la asilimia 9.2 ikilinganishwa na kiasi kilicholipwa kwa wakulima hao mwaka wa fedha uliotangulia.

Mahitaji ya sukari nchini ni jumla ya tani 570,000 wakati viwanda vya ndani vina uwezo wa kuzalisha tani 320,000. “Ili kufidia pengo hilo serikali imekuwa ikitoa kibari kwa wafanyabiashara kuagiza lakini baadhi yao wamekuwa si waminifu. Wanaagiza sukari zaidi na kuingiza nchi kupitia njia za panya hivyo kuathiri wazalishaji wa ndani”, alisema. 

Pinda alisema serikali inatambua juhudi zinazofanywa na kiwanda hicho kwa ajili ya maslahi ya jamii inayoizunguka. “Hospitali mpya ambayo imejengwa hivi karibuni imekuwa ni msaada mkubwa kwa wakazi wa Kidatu, Kilombero na maeneo ya jirani na hivyo kuepusha adha ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya,” alisema.

Kiwanda cha Sukari cha Kilombero kimewekeza zaidi ya shilingi milioni 700 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ambayo kwa sasa inatoa huduma mbalimbali za afya kama vile X-ray, upasuaji, uvimbe, afya ya mama mjamzito na  mototo mchanga.

Alisema Kiwanda cha Kilombero ni miongoni mwa maeneo yanayolipa kodi kubwa sana nchini. “Katika mwaka wa fedha uliopita, kiwanda cha Kilombero kichangia zaidi ya shilingi milioni 22 kwa serikali kupitia kodi mbalimbali.

Mapema katika hotuba yake ya utambulisho, Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha cha Sukari cha Kilombero Bw. Mark Bainbridge alielezea kuridhishwa kwake na sapoti kutoka kwa serikali na kuahidi kuendelea kutoa bidhaa zenye ubora wa hali ya juu. “Kwa miaka zaidi ya ishirini, Kiwanda cha Sukari  kilombero kimekuwa kikifanya biashara zake nchini kwa rekodi nzuri.

“Maamuzi yetu ya kuwa na muonekano mpya wa Bwana Sukari yanatokana na utafiti wetu wa kina tuliofanya hivi karibuni ambao umeoyesha kwamba sukari yetu inapendwa na Watanzania wengi kutokana na u bora uliopo. Tunataka kuendeleza imani hii na kuthibitisha uwepo na nia yetu kuendelea kuwa hapa na kulinda biashara yetu dhidi ya watu yenye nia ya kuchafua jina la kampuni kwa wateja wetu,” alisema.

Alisema kampeni hii  itatangazwa kupitia TV, radio, magazeti, vyombo vya kidigitali na sampuli mbalimbali. “Lengo yetu ni kuhakikisha ujumbe kuhusu sura mpya ya Bwana Sukari unawasilishwa vizuri na kueleweka vizuri kwa kila mmoja,”alisema

Bidhaa ya Bwana Sukari imekuwa ni maarufu sana katika mikoa ya Morogoro, Iringa, Mbeya, Dodoma na Dar es Salaam ambako inauzwa sambamba na bidhaa nyingine.
Posted by MROKI On Thursday, October 22, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo