Michuano ya mpira wa Pete (Netball) Taifa yanaendelea katika viwanja vya Sigara Changombe Jijini Dar es salaam na leo hii jioni palishuhudiwa mchezo kati ya Dodoma na Kinondoni ambapo mashabiki wa mvchezo huo walishuhudia Dodoma ikishusha kichapo kingine kwa vibonde kinondoni kwa mabao 35-17.
Pichani juu ni Dodoma (zambarau) wakicheza gonga za kuwapoteza Kinondoni uwanjani.
Hesabu zilihitajika ili kufunga vyema.
Mfungaji bora wa mabao ya Dodoma, Lupondo Lweli (GS) akipachika moja ya mabao yake.
Benchi la Kinondoni lilikuwa ni majonzi.
Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Mara, Ester Bulaya (kulia) walikuwa wakishangilia timu tofauti. Ester alishangilia Dodoma. Katikati ni Anna Kibira wa CHANETA.
Hadi Mapumziko Dodoma ilikuwa mbele kwa mabao 17-10 ya Kinondoni.
Wachezaji wanapo potezana na mpira ulionasa katikati ya miguu yao.
Nipatashika ya mnguo kuchinaka katika mchezo huo.
Lupondo Lweli ndiye aliyeongoza kipondo cha Kinondoni kwa kupachika magoli mengi katika mchezo huo.
No comments:
Post a Comment