KESHO ni siku ya Siku kuu,
pasi na shaka hakuna mtu ambaye halijui hilo.
Siku kuu ya Krisimasi na mwaka mpya ni siku kuu
ambazo hufuatana na kwadesturi ya ushirikiano tulio nao hapa nchini siku hizi
hatubagui hatuchagui kila mtu hufurahi pamoja na mwenzake.
Furaha hii ni pale wana jamii walio na mirengo
tofauti ya kiimani wanapojumuika pamoja na kufurahia, waumini wa dini ya
Kikristo walio wengi kesho wanasherehekea kuzaliwa kwa Masia Yesu Kristo.
Lakini kidoogo tujikumbushe kuzaliwa kwa Yesu
Kiristo kulikuaje; Maandiko matakatifu kutoka katika Kitabu cha Biblia Matayo
1:18-21 kunaelezea wazi namna Yesu Kristo alivyo zaliwa.
Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi: Maria
mama yake, alikuwa ameposwa na Yosefu. Lakini kabla ya ndoa yao, Maria akiwa
bado bikira, alipata mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu.
Kwa kuwa Yosefu alikuwa mtu mwema hakutaka
kumwaibisha mchumba wake Maria hadharani. Kwa hiyo aliamua kuvunja uchumba wao
kwa siri. Lakini alipokuwa bado anawaza juu ya jambo hili, malaika wa Bwana
akamtokea katika ndoto akasema, “Yosefu mwana wa Daudi, usisite kumwoa Maria
mchumba wako kwa maana mimba aliyo nayo ameipata kwa uweza wa Roho Mtakatifu.
Naye atamzaa mtoto wa kiume, nawe utamwita jina
lake Yesu; kwa maana yeye ndiye atakayewaokoa watu wake kutoka katika dhambi
zao.”
Tangu kuzaliwa kwa kristo yapata miaka 2000 sasa
na kwa kawaida husheherekewa tarehe 25 Desemba katika Ukristo wa magharibi na
tarehe 6 Januari katika ule wa mashariki.
Hii ni siku ambayo wazazi na watoto wao hukaa
pamoja na kufurahi kwa kula na kunywa vinono huku watoto tayari wakiwa
wamevalia nadhifu na kufurahi. Siku hizi hata waislamu huwapendezesha watoto
wao na wao wenye katika siku hii maana nao hupata mialiko kwa ndugu na jamaa
zao kufurahi pamoja.
Leo Anko Kidevu nitazungumzia ulinzi wa familia
zetu katika siku hii. Ni dhahiri kuwa tulivyo amka salama asubuhi basi sote
tunatamani pakuchwe salama.
Tutokapo asubuhi salama majumbani mwetu pasi na
shaka kuwa wale tuliowaacha majumbani wanatamani turudi salama na furaha
kuzidi.
Tupo wazazi ambao tutawaruhusu watoto wetu
kuzunguka mahali hapa na pale kutimiza furaha zao. Tupo wazazi ambao tutaenda
na watoto wetu katika fukwe na katika majumba makubwa ya kibiashara palipo na
maduka na michezo ya watoto.
Angalizo langu tu ni kuwa na makini na watoto
wetu hata na kila mtu mzima amwangalie mwenzake pia tusije tukapotezana ama kwa
kugongwa na magari, kuzama majini au kupotea katika mazingira tatanishi.
Pia ningependa kuvisihi sana vyombo vya dola
hasa vya ulinzi na usalama wa raia na mali zao, tuyaangalie maeneo yote ya
mikusanyiko kwa jicho la tatu.
Siwafundishi kazi katika hili, ila panapojaliwa
wasaa wa kukumbushana ni vyema tukakumbushana maana ulinzi na usalama ni wetu
sote.
Jicho la tatu linahitajika sana hasa katika majumba
makubwa ya biashara kama, Mlimani City, Quality Center, Shopaz Plaza, May Fair
Plaza na kwingineko kote ambako wahuni wachache wanaweza tumia mwanya huo na
kututia mchanga katika pilau letu.
Kidevu nilipita katika moja ya majengo hayo leo,
lakini nilishangaa ulinzi uliokuwapo siku za nyuma baada ya tukio Septemba 21, 2013,
pale katika jingo la Westgate jijini Nairobi, Kenya ambako watu wasio julikana
walivamia na kufanya dhahama iliyo gharimu uhai wa watu maduka yetu yalikuwa na
ulinzi na uingiapo unakaguliwa lakini sasa naona haupo tena.
Si kweli kuwa wahalaifu wamelala bali wanatusoma
tu, hivyo tuwe makini na turejeshe ulinzi katika majengo hayo.
Niimani yangu kuwa wote pia tutabeba jukumu lakuhakikisha
usalama wetu unakuwepo kwa watumiaji wa vileo kunywa karibu na nyumbani na
kuepuka kutumia vyombo vya moto tukiwa tumelewa.
Watoto wasiende kucheza mbali na nyumbani,
tutakao pata wasaa tuingie ibadani na kuwatembelea wagonjwa mahospitalini
kuwapa faraja.
Anko Kidevu sina la zaidi bali nawatakia siku
kuu njema ya X Mass na Mwaka mpya pia.
AMANI YETU -USALAMA WETU NDIO FURAHA YETU
No comments:
Post a Comment