Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akikabidhi vyakula mbalimbali kwa Bi. Honorata wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Honorata kilichopo Temeke jijini Dar es salaam leo wakati alipokabidhi msaada wa vyakula kwa vituo mbalimbali vya jijini Dar es salaam ikiwa ni zawadi yake ya sikukuu ya Krismas kwa vituo hivyo, Bw. Alex Msama amesema pia katika Tamasha la Pasaka litakalofanyika kesho wakati wa sikukuu ya Krismas mkoani Mbeya, kiasi cha fedha zitakazopatikana zitakwenda kulipia ada za watoto yatima katika vituo mbalimbali vitakavyofikiwa na msaada huo, Ameongeza kwamba msaada huo wa vyakula una thamani ya shilingi milioni Nne na Nusu. Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akikabidhi vyakula mbalimbali kwa Bi. Halima Mpeta wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Mwandaliwa kilichopo Mbweni jijini Dar es salaam. Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akikabidhi vyakula mbalimbali kwa Bw. Rashid Mpinda katibu wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Maunga Centre cha Kinondoni. Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akigwa vyakula mbalimbali baada ya kukabidhi kwa vituo vya kulelea watoto yatima jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akifafanua jambo kwa wanahabari mara baada ya kukabidhi msaada wa vyakula kwa vituo vya kulelea watoto yatimajijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment