Meneja
wa ATM na Kadi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Wambura John
(kushoto) akiweka pesa kwa kutumia ATM katika hafla ya uzinduzi wa
huduma ya kuweka pesa (deposit) kwa kutumia mashine za ATM ya benki ya
NBC jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katikati ni mteja wa benki
hiyo, Francis Xavier na kulia ni Meneja Huduma za Jamii wa NBC, Irene
Peter
Mteja
wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Francis Xavier (kushoto) akiweka
pesa (deposit) katika mashine ya ATM ya benki hiyo wakati wa uzinduzi
rasmi wa huduma hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katikati
ni Meneja wa ATM na Kadi wa NBC, Wambura John (katikati) na Meneja
Huduma za Jamii wa benki hiyo, Irene Peter.
BENKI
ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma mpya ya kuweka fedha kwenye
mashine za ATM jijini Dar es Salaam katika juhudi za benki hiyo
kuboresha huduma za kifedha nchini.
Kuanzishwa
kwa huduma hiyo kunathibitisha malengo ya benki hiyo ya kutoa huduma
sahihi na ya wakati kwa wateja wake nchini nzima na huduma hii ya kuweka
fedha kwenye mashine za ATM itakuwa ikipatikana masaa 24 kila siku.
No comments:
Post a Comment