Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima (kushoto) akimkabidhi
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Rished Bade Ngao ya ushindi wa kwanza
kwa taasisi za serikali kwa kuweka kumbukumbu za mahesabu vizuri mwaka
2013/14 inayotambuliwa na Bodi ya Wakaguzi wa Mahesabu nchini (NBAA), juzi
mkoani Arusha, wanaoshudia ni wafanyakazi wa TRA.
Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima akifurahia jambo na Kamishna Mkuu wa TRA Rished Bade. Picha ya pamoja.
Na Mwandishi Wetu
Taasisi za serikali, mashirika ya umma wizara na idara mbalimbali za serikali zimeshauriwa kushiriki
katika mashindano ya uwasilishaji wa taarifa bora za fedha za mwaka tofauti na ilivyo sasa ambapo makundi haya
yamekuwa yakishiriki kwa uchache sana na sehemu kubwa ya washiriki kuachiwa taasisi na mashirika binafsi.
Akizungumza wakati
wa hafla ya utoaji tuzo na vyeti kwa washindi
katika uwasilishaji wa taarifa
bora za fedha mwaka 2014, Naibu Waziri
wa Fedha, Adamu Malima amesema ni wakati mwafaka kwa taasisi na idara mbalimbali za serikali
kuingia katika mashindano hayo ili kujipima na kuongeza ufanisi katika utunzaji
na uandaaji wa taarifa zao kulingana na viwango vya kimataifa IFRS.
Katika
mshindano hayo ambayo huratibiwa na
bodi ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu nchini NBAA kwa mwaka huu jumla
ya washiriki 40 walishiriki ambapo
mamlaka ya mapato nchini TRA Iliibuka mshindi wa kwanza kwa
uwasilishaji wa taarifa bora za fedha kwa mwaka 2013 -2014. kwa upande
wa
taasisi za serikali.
No comments:
Post a Comment