December 06, 2014

SHULE YA AWALI YA ABEL MEMORIAL NURSERY AND PRIMARY SCHOOL YAFANYA MAHAFALI YAKE HII LEO

Wahitimu wakiwa katika pozi za kusubiri sherehe ya kuwaaga rasmi kutoka elimu ya awali kuingia elimu ya msingi
Mgeni rasmi wa mahafali hayo mama NEEMA KIBANGA ambaye ni afisa elimu wa kata ya bunju akikabidhi vyeti kwa wahitimu shuleni hapo

Wahitimu wakiwa katika picha ya pamoja na walimu wao baada ya kukabidhiwa vyeti vyao
Mmoja wa wamiliki wa shule hiyo ambaye ni mke wa meneja wa shule hiyo BI ROSE MWALONGO akizungumzas na watoto wa shule hiyo mapema kabla ya kuanza shughuli rasmi ya mahafali ya shule hiyo
******
  Na Exaud Mtei
Shule ya wanafunzi wa awali ya ABEL MEMORIAL NURSERY AND PRIMARY SCHOOL leo imefanya mahafali ya wanafunzi wa awali wanaovuka kuingia elimu ya msingi huku ikiwa na mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwake shule hiyo mnamo mwaka 2012.
Shule hiyo ambayo inapatikana BUNJU jijini Dare s salaam ambayo ilianza mwaka 2012 ikiwa na jumla ya watoto tisa tu na mwalimu mmoja ambapo mwaka 2013 idadi iliongezeka na kufikia watoto 13 na hatimaye mwaka huu wa 2014 shule hiyo ina watoto 31 pamoja na walimu wawili jambo ambalo limetajwa kuwa ni mafanikio makubwa kwa shule ya watoto iliyoanzishwa na watanzania wazalendo kwa ajili ya kuinua elimu ya watoto wa Tanzania.
Akizungumza katika mahafali ya shule hiyo leo meneja wa shule hiyo Bwana STANSLAUS ABED MWALONGO amesema kuwa lengo lilikuwa ni kuanzisha shule ya secondary lakini baada ya kutafakari kwa kina akaona ni vyema kuanzisha shule ya awali na msingi ili kutoa msingi bora wa elimu kwa watoto wetu.

No comments:

Post a Comment