December 06, 2014

KIIZA AIBEBA YANGA KWA GOLI LA 'FAIRPLAY' DHIDI YA EXPRESS YA UGANDA

 Mabingwa mara 24 wa soka la Tanzania, Yanga ya Dar es Salaam imewazamisha Express ya Uganda kwa goli 1-0 lilifungwa katika dakika ya 90 kufuatia mpira wa kurushwa uliotolewa nje baada ya mchezaji wa Xpress ya Uganda kuumia.

Mchezaji wa kulipwa wa Uganda, Hamisi Kiiza anaekipia na Yanga ndiye aliyepachika goli hilo ambalo hata hivyo lilionesha kulalamikiwa na benchi la ufundi la Express ambao walikuwa wakihoji tunawafundisha nini wachezaji juu ya Fair Play?
Wachezaji wakiwania mpira wakati wa mchezo huo wa kimataifa wa kirafiki uliopigwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam hii leo na Express waliotoka suluhu na Simba juzi a bao 0-0 waliambulia kichapo cha 1-0 kutoka Yanga.

No comments:

Post a Comment