December 23, 2014

MISS TANZANIA 2013 HAPPINES WATIMANYWA AREJEA NYUMBANI LEO

Miss Tanzania 2013, Hapopiness Watimanywa (kushoto) amerejea hii leo akitokea jiji London Uingereza alikokuwa akishiriki mashindano ya Miss World 2014. 

Watimanywa akizungumza na Father Kidevu Blog hii leo asubuhi baada ya kuwasili uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na Kupokelewa na Miss Tanzania 2014, Lilian Kamazima (Pichani kulia), Viongozi wa Kamati ya Miss Tanzania pamoja na familia yake alisema kuwa licha ya kuwa yeye hakufanya vyema katika mashindano hayo lakini amefurahi taji hilo kuja Afrika.

Aidha Watimanywa amewaasa warembo wenzake hasa Lilian Kamazima anaetaraji kwenda katika mashindano hayo mwakani kutumia zaidi kujichanganya katika mitandao ya kijamii kama facebook, Twitter na Instagram ili kujipatia kura nyingi hapo baade. 

Happiness akilakiwa na wadogo zake Angela Roussos na Romeo baada ya kuwasili hii leo asubuhi.
Happiness akipokelewa mizigo na baba yake, Lous Rousso.
Mkurugenzi wa Lino Intenational Agency, waandaaji wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga akimsalimia Happiness Watimanywa. Kulia ni baba yake, Lous Rousso
Happiness Watimanywa akiwa na Mama yake Amina Bukoko.
Happiness akizungumza na familia yake uwanjani hapo.
Picha ya pamoja ya wote waliofika kumpokea Happiness Watimanywa.

No comments:

Post a Comment