Na Andrew Chale
WABUNIFU wa Mavazi wachanga na chipukizi wamemwandalia
Sherehe za kuzaliwa ya Mama wa Mitindo, Asia Idarous Khamsin, zitakazofanyika
usiku wa Desemba 24, ndani ya ukumbi wa M.O.G Bar (Nyumbani Lounge) huku
ikisindikizwa na Spice Modern Taarab pamoja na Mini fashion show.
Katika usiku huo maalum, kiingilio ni sh 5,000, huku vazi
maalum likiwa Black & White, ambapo pia wadau watakaojumuika na Mama wa
Mitindo, watapata burudani kali ya muziki kutoka kundi hilo la Spice Modern
taarab, Dj Mapuu pamoja na shoo ya
ubunifu wa mavazi (Min fashion show) itakayopambwa na wabunifu wanaochipukia.
Usiku huo wa Black &White Bash 55th Asia Idarous Khamsin, pia itakuwa na Red Carpet
na wadau watapiga picha na mastaa mbalimbali sambamba na pongezi za kunyakua
tuzo ya ‘Life Time Achievement Swahili Fashion Week 2014’.
No comments:
Post a Comment